Malalamiko dhidi ya matamshi ya kukejeli Uislamu nchini Uingereza
(last modified Thu, 09 Aug 2018 02:28:27 GMT )
Aug 09, 2018 02:28 UTC
  • Malalamiko dhidi ya matamshi ya kukejeli Uislamu nchini Uingereza

Katika mkondo wa wimbi la kupinga matamshi ya dharau na kebehi yaliyotolewa na waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Uingereza dhidi ya Waislamu, Mwenyekiti wa chama cha Conservative cha Uingereza amemtaka Boris Johnson aombe radhi kutokana na matamshi yake dhidi ya wanawake wa Kiislamu wanaovaa vazi la burqa.

Hivi karibuni Johson aliwafananisha wanawake Waislamu wanaotumia vazi la Niqab au burqa na majambazi wanaoiba kwenye mabenki. Alieleza uungaji mkono wake kwa marufuku ya vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu hijabu katika maeneo ya umma na kulitaja kuwa ni kichekecho. 

Matamshi hayo ya waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Uingereza yametolewa katika hali ambayo katika miezi ya hivi karibuni kumenzishwa mashambulizi makali dhidi ya Waislamu hususan wanawake wa Kiislamu wanaovaa vazi la hijabu katika nchi za Ulaya. Wanawake hao wa Kiislamu ambao wanakabiliwa na athari mbaya za hujuma zinazofanywa dhidi ya matukufu ya dini yao na hata ubaguzi wa kijamii katika jamii ya Ulaya ikiwa ni pamoja na katika maeneo ya kazi na katika mishahara. Kwa mujibu wa ripoti ya ripoti ya Kituo cha Nyaraka na Ushauri katika Masuala ya Waislamu nchini Austria, katika miaka ya hivi karibuni wanawake wa Kiislamu wamekuwa wahanga wa hujuma dhidi ya Uislamu barani Ulaya kwa kadiri kwamba, wanaunda asilimia 98 ya Waislamu walioshambuliwa.

Boris Johnson 

Hojjat Ramzi ambaye ni afisa wa taasisi inayofuatilia hujuma na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu nchini Uingereza ya Tell MAMA anasema: Hali ya Waislamu nchini Uingereza imekuwa mbaya zaidi katika upande wa hujuma zinazolenga wafuasi wa dini hiyo.

Ongezeko la wahajiri Waislamu kutoka nchi za magharibi mwa Asia kuelekea Ulaya, vitisho vya mashambulizi ya kigaidi katika nchi za Ulaya, kunasibishwa kwa Waislamu, na harakati haribifu na za kichochezi za vyombo vya habari ambavyo vinayahusisha matatizo na mashambulizi mengi ya kigaidi na Waislamu, vimewafanya wafuasi wengi wa dini hiyo wakabiliwe na mashambulizi ya mara kwa mara ya makundi ya wabaguzi wenye chuki dhidi ya Uislamu. Misimamo hii imeshadidi zaidi baada ya vyama vyenye misimamo mikali vya mrengo wa kulia kushika hatamu za uongozi katika baadhi ya nchi za Ulaya. Huko Uingerea pia wanachama wa chama cha Conservative wanaounda barala la mawaziri la serikali ya Theresa May wamezidisha chuki na hujuma dhidi ya Uislamu na wanatumia suala hilo kama wenzo wa kuimarisah nguvu yao ya kisiasa na kwa ajili ya kupata kura za wafuasi wa makundi yenye misimamo mikali katika chaguzi mbalimbali.

Sayeeda Warsi, aliyekuwa naibu wa mkuu wa zamani wa chama cha Conservative amesema kuwa Johnson amefanya hivyo kwa makusudi ili kupata uungaji mkono wa mrengo wa kulia wenye misimamo mikali.

Kutokana na hali hiyo ya kuongezeka hujuma na chuki za wanasiasa wa Uingereza dhidi ya Uislamu na Waislamu Baraza la Waislamu la nchi hiyo limetoa wito rasmi wa kufanyika uchunguzi kuhusu hujuma hizo ndani ya chama cha Conservative.

Alaa kulli hali matamshi yalitotolewa na Boris Johnson yameonesha tena kwamba, japokuwa serikali ya Uingereza imeahidi walau kidhahiri na kwa maneno tu kwamba itakabiliana na hujuma na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu lakini kivitendo haichakukua hatua yoyote ya maana kupunguza jinai za aina hiyo. Si hayo tu bali wanasiasa wa nchi hiyo wameendelea kuchochea moto wa hujuma na mashambulizi makali dhidi ya Waislamu.

Tags