Putin ataka jeshi la Russia lipewe kizazi kipya cha silaha
https://parstoday.ir/sw/news/world-i48267-putin_ataka_jeshi_la_russia_lipewe_kizazi_kipya_cha_silaha
Rais Vladmir Putin wa Russia amesisitiza udharura wa kukabidhiwa jeshi la nchi hiyo kizazi kipya cha silaha kwa ajili ya kulifanya jeshi hilo kuwa bora zaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 20, 2018 10:44 UTC
  • Putin ataka jeshi la Russia lipewe kizazi kipya cha silaha

Rais Vladmir Putin wa Russia amesisitiza udharura wa kukabidhiwa jeshi la nchi hiyo kizazi kipya cha silaha kwa ajili ya kulifanya jeshi hilo kuwa bora zaidi.

Putin ameyasema hayo katika kikao cha Kamisheni ya Viwanda vya Zana za Ulinzi na kusisitiza kuwa, kuna udharura wa kukabidhiwa ndege mpya za kijeshi za kizazi cha tano aina ya Sukhoi Su-57, vifaru vipya aina ya Armata, makombora ya kuvuka mabara aina ya Sarmat na ngao ya makombora ya S 500 kwa jeshi la Russia.

Rais Vladmir Putin akikagua aina mpya ya kizazi kipya cha silaha

Aidha Putin na katika siku ya kuwaenzi waunda silaha wa nchi yake katika maonyesho ya silaha za kijeshi, ametembelea eneo la Patriot la Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo katika wilaya ya Kubinka ya mji mkuu, Moscow ambapo amekagua aina mbalimbali ya kizazi kipya cha silaha zilizoundwa nchini humo.

Rais Vladmir Putin wa Russia pia ametembelea maonyesho ya silaha zikiwemo silaha na zana za kijeshi tofauti zinazomilikiwa na jeshi la nchi yake. Itakumbukwa kuwa moja ya kaulimbiu za Putin katika kampeni za uchaguzi wa rais uliopita nchini Russia ni kulijenga upya jeshi la nchi hiyo ili kukabiliana na vitisho vya kambi ya adui.