Kiongozi wa upinzani nchini Russia atiwa mbaroni kwa mara nyingine
https://parstoday.ir/sw/news/world-i48367-kiongozi_wa_upinzani_nchini_russia_atiwa_mbaroni_kwa_mara_nyingine
Kiongozi wa upinzani nchini Russia ametiwa mbaroni kwa mara nyingine baada ya kushikiliwa kwa muda wa mwezi mmoja na kuachiliwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 24, 2018 22:53 UTC
  • Kiongozi wa upinzani nchini Russia atiwa mbaroni kwa mara nyingine

Kiongozi wa upinzani nchini Russia ametiwa mbaroni kwa mara nyingine baada ya kushikiliwa kwa muda wa mwezi mmoja na kuachiliwa.

Alexei Navalny amepelekwa katika makao makuu ya polisi ya wilaya ya Danilovsky ya mjini wa Moscow, ambapo anakabiliwa na tuhuma mpya za kuitisha maandamano ya nchi nzima dhidi ya serikali. Mwezi mmoja uliopita Navalny alitiwa nguvuni kwa kuratibu maandamano ya kijamii wakati wa kujiri mashindano ya kombe la dunia na pia kulalamikia sheria mpya ya kustaafu nchini humo.

Rais Vladmir Putin wa Russia

Inaelezwa kwamba huenda Alexei Navalny akatakiwa kulipa kiasi cha Ruble laki tatu, ambazo ni sawa na Dola 4500 au kuhukumiwa kifungo cha siku 20 jela. Hukumu ya mwisho dhidi ya mwanasiasa huyo ilikuwa kifungo cha siku 30 ambayo ilitolewa mwezi Mei mwaka huu kwa tuhuma za kuitisha maandamano dhidi ya serikali ya Rais Vladmir Putin. Baadhi ya duru zinaarifu kwamba, Alexei Navalny ana mfungamano wa kisiasa na kiuchumi na baadhi ya serikali za Magharibi katika harakati zake.