Korea Kaskazini: Japan inakusudia kurejesha mfumo wa kijeshi katika eneo
(last modified Thu, 18 Oct 2018 08:04:24 GMT )
Oct 18, 2018 08:04 UTC
  • Korea Kaskazini: Japan inakusudia kurejesha mfumo wa kijeshi katika eneo

Serikali ya Korea Kaskazini imekosoa azma ya Japan ya kuelekea kwenye mfumo wa kijeshi kwamba, kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo ni kurejesha kipindi kilichopita cha umwagaji damu.

Gazeti rasmi la serikali ya Korea Kaskazini la Rodong Sinmun sambamba na kukosoa mpango wa kuifanyia marekebisho katiba ya Japan kwa ajili ya kufungua njia ya kutuma askari wa nchi hiyo kushiriki katika operesheni nje ya mipaka yake, limeandika kuwa, hatua hiyo ni tishio kwa eneo lote la Asia.

Askari wa Japan

Kwa mujibu wa gazeti hilo, mpango huo ni sawa na kuhuisha upya kipindi cha umwagaji damu katika eneo. Gazeti hilo limezidi kufafanua kuwa, hatua ya Shinzo Abe, Waziri Mkuu wa Japan ya kuendelea kusisitiza umuhimu wa kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo inakusudia kufufua kipindi cha kijeshi. Abe ametangaza kwamba, katika njia ya kuifanya Japan kuwa mpya atahakikisha anaifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo. Lengo kuu ni kuwaruhusu askari wa nchi hiyo kuweza kushiriki katika operesheni nje ya mipaka ya Japan kutokana na mazingira ya sasa ya dunia. Shinzo Abe, ambaye atakuwa madarakani hadi mwaka 2020, anaonekana kuwa aliyejikita sana katika suala la kuifanyia marekebisho katiba, kwa lengo la kufufua uwezo wa jeshi la nchi hiyo ya Asia Mashariki.

Tags