Lavrov atahadharisha kuhusu hatari ya ugaidi duniani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i49367-lavrov_atahadharisha_kuhusu_hatari_ya_ugaidi_duniani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema ugaidi ungali upo kote ulimwenguni na ni jambo la hatari kwa nchi zote licha ya mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya janga hilo.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Nov 08, 2018 08:25 UTC
  • Lavrov atahadharisha kuhusu hatari ya ugaidi duniani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema ugaidi ungali upo kote ulimwenguni na ni jambo la hatari kwa nchi zote licha ya mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya janga hilo.

Sergei Lavrov ameongeza kuwa, makundi ya kigaidi yanaimarisha vyanzo vyao vya kifedha na teknolojia zao kupitia harakati kubwa za madawa ya kulevya na jinai zilizoratibiwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia aliyasema hayo katika kikao cha kimataifa cha taasisi za itelijinsia duniani huko Moscow mji mkuu wa Russia jana Jumatano. Lavrov amesema kuwa magaidi huko  Syria na Iraq wanaendelea kupata misaada kutoka nje ikiwemo misaada ya silaha. Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia ameongeza kusema kuwa nguvu ya makundi ya kigaidi imedhoofika sana, hata hivyo harakati zao katika eneo la Mashariki ya Kat bado hazijasambaratishwa kikamilifu kutokana na uungaji mkono wa nchi ajinabi kwa magaidi hao ukiwemo wa misaada ya silaha kwa makundi hayo. 

Magaidi wa Daesh nchini Iraq

Lavrov ametoa wito wa kuwepo ushirikiano wa maana wa kimataifa na ulio wazi ikiwa ni pamoja na katika masuala ya kisheria na kupeana taarifa kwa wakati kuhusu harakati za magaidi.