Russia na OIC zakubaliana kushirikiana katika vita dhidi ya ugaidi
Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na pande mbili kukubaliana juu ya kushirikiana katika kupambana na ugaidi.
Oleg Syromolotov, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema katika mazungumzo yake na Abdullah Alim, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC pamoja na ujumbe aliaofuatana nao ambapo wawili hao wameafikiana juu ya kutawisha ushirikiano wao katika suala zima la kupambana na ugaidi.
Oleg Syromolotov, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia na Abdullah Alim, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC wamejadili na kukubaliana pia juu ya kuweko ushirikiano wa kimataifa katika vita dhidi ya ugaidi na misimamo ya kufurutu ada.
Tishio la ugaidi katika maeneo mbalimbali ulimwenguni likiwemo eneo la Mashariki ya Kati pamoja na mbinu na mikakati ya kukabiliana nao ni miongoni mwa zilizokuwa ajenda za mazuungumzo kati ya pande mbili hizo.
Russia imekuwa mwanachama mtazamaji wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC tangu mwaka 2015.
Madola ya Magharibi hususan Marekani yamekuwa yakikosolewa kutokana na undumakuwili wao katika vita dhidi ya ugaidi na hata kkuuuagawa ugaidi katika makundi mawili ya ugaidi mzuri na mbaya. Aidha baadhi ya nchi za Kiarabu kama Sauudi Arabia nazo zinaandamwa na ukosoaji kutokana na kuyyaunga mkono na kuyasaidia kifedha makundi ya kigaidi.