Chuki dhidi ya Waisraeli yaongezeka kwa 74% nchini Ufaransa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i51515-chuki_dhidi_ya_waisraeli_yaongezeka_kwa_74_nchini_ufaransa
Serikali ya Ufaransa imesema vitendo na matamshi ya chuki dhidi ya Mayahudi wanaoishi katika nchi hiyo ya Ulaya yameongezeka kwa asilimia 74, rekodi ambayo haijawahi kushuhudiwa tena.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 12, 2019 23:02 UTC
  • Chuki dhidi ya Waisraeli yaongezeka kwa 74% nchini Ufaransa

Serikali ya Ufaransa imesema vitendo na matamshi ya chuki dhidi ya Mayahudi wanaoishi katika nchi hiyo ya Ulaya yameongezeka kwa asilimia 74, rekodi ambayo haijawahi kushuhudiwa tena.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Christophe Castaner amekiri kuwa, chuki dhidi ya Mayahudi nchini humo imeongezeka kwa kiwango cha kutisha, na  kuwa inasambaa katika kila kona ya nchi kama sumu ya nyoka.

Vyombo vya usalama nchini Ufaransa vimeripoti kuwa, visa vya chuki dhidi ya watu wenye asili ya utawala wa Kizayuni wa Israel nchini humo vilivyorekodiwa mwaka jana 2018 ni 541, ikilinganishwa na 311 mwaka 2017.

Afisa wa Idara ya Mahakama ambaye hakutaka kutaja jina lake ameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa, Waendesha Mashitaka mjini Paris wanachunguza matukio manne ya kushambuliwa Mayahudi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu

Amesema matukio hayo manne ni sehemu ya mamia ya visa hivyo vilivyorekodiwa katika kipindi cha miezi michache iliyopita.

Ufaransa inatajwa kuwa nchi yenye idadi kubwa zaidi ya wahamiaji wa Kiyahudi baada ya Marekani. Utawala ghasibu wa Israel hivi sasa unaendelea kupora na kukalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina.