Uchunguzi: Waislamu wanabaguliwa zaidi katika jamii ya Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i52059-uchunguzi_waislamu_wanabaguliwa_zaidi_katika_jamii_ya_marekani
Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanyika nchini Marekani yanaonesha kuwa, Waislamu wanabaguliwa zaidi katika jamii ya nchi hiyo ikilinganishwa na makundi mengine ya kidini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 09, 2019 21:47 UTC
  • Uchunguzi: Waislamu wanabaguliwa zaidi katika jamii ya Marekani

Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanyika nchini Marekani yanaonesha kuwa, Waislamu wanabaguliwa zaidi katika jamii ya nchi hiyo ikilinganishwa na makundi mengine ya kidini.

Matokeo ya uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na taasisi ya Hill-HarrisX yanaonesha kuwa, asilimia 85 ya walioshiriki katika uchunguzi huo wanaamini kuwa, Waislamu wanasumbuliwa na ubaguzi mkubwa zaidi katika jamii ya Marekani kuliko makundi mengine ya kidini.

Uchunguzi huo wa maoni unaonesha kuwa, asilimia 61 ya Wamarekani Wakristo pia wanabaguliwa nchini humo. 

Matokeo ya uchunguzi huyo yametolewa baada ya Kongresi ya Marekani kupasisha azimio lililolaani hujuma ya propaganda za kuchafua jina la dini ya Uislamu na vitendo vingine vya chuki na uadui dhidi ya Waislamu. 

Ripoti za awali zilionesha kuwa, robo ya kesi za ubaguzi zilizowasilishwa katika vyombo husika nchini Marekani zilihusiana na ubaguzi unaofanyika dhidi ya Waislamu katika ajira nchini humo. 

Kamisheni ya Fursa Sawa za Ajira nchini Marekani (EEOC) imeripoti kuwa, katika kipindi cha miezi 9 ya kwanza ya mwaka 2009 tu wafanyakazi Waislamu waliwasilisha kesi zaidi ya 800 zilizohusiana na kubaguliwa katika maeneo ya kazi na kwamba kiwango hicho kimeongezeka kwa asilimia 20 ikilinganishwa na mwaka 2007.