Korea Kaskazini yaiwekea Marekani sharti ili kurejea kwenye mazungumzo
(last modified Sun, 26 May 2019 02:28:05 GMT )
May 26, 2019 02:28 UTC
  • Korea Kaskazini yaiwekea Marekani sharti ili kurejea kwenye mazungumzo

Serikali ya Korea Kaskazini imesema kuwa sharti la Pyongyang la kurejea kwenye meza ya mazungumzo na Marekani ni serikali ya Washington kubadilisha siasa zake za upande mmoja.

Shirika rasmi la Habari la Korea Kaskazini limeinukuu Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo akisema kuwa, madamu serikali ya Marekani haijaachana na matakwa yake ya upande mmoja katika mwenendo wa mazungumzo kuhusiana na kadhia ya kuangamiza silaha za nyuklia, basi Pyongyang haitorejea kwenye mazungumzo hayo. Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini imetaja sababu ya kuvunjika mazungumzo ya mwezi Februari mjini Hanoi, Vietnam kati ya Donald Trump na Kim Jong-un kuwa ilitokana na hatua ya Washington kuwasilisha matakwa ya upande mmoja na yasiyowezekana.

Marekani, nchi isiyoaminika kufanya nayo mazungumzo

Hii ni katika hali ambayo kiongozi wa Korea Kaskazini (Kim Jong-un) ameipatia Marekani muhula wa hadi mwishoni mwa mwaka huu kuhakikisha inaachana na mienendo yake hasi dhidi ya Pyongyang ili kurejea kwenye mazungumzo ya pande mbili. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, iwapo Marekani itatekeleza sharti hilo, itawezekana kufikiwa makubaliano katika mazungumzo hayo.

Tags