Federica Mogherini asisitiza kulindwa makubaliano ya JCPOA
(last modified Thu, 20 Jun 2019 07:33:21 GMT )
Jun 20, 2019 07:33 UTC
  • Federica Mogherini asisitiza kulindwa makubaliano ya JCPOA

Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya amesisitiza kulindwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Federica Mogherini ametoa taarifa pambizoni mwa ziara yake huko Marekani katika mazungumzo na Mike Pompeo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hiyo akisema kuwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA ni wenzo muhimu katika kulinda amani na uthabiti katika eneo. 

Taarifa ya Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya imeendelea kubainisha kuwa umoja huo unahimiza kulindwa makubaliano hayo ya nyuklia na Iran; na kwamba Umoja wa Ulaya unayatambua makubaliano hayo kuwa ni wenzo muhimu katika kulinda amani na uthabiti katika eneo. Rais Donald Trump wa Marekani tarehe Nane Mei mwaka jana alichukua uamuzi wa upande mmoja na kujitoa kwenye makubaliano hayo ya kimataifa na kisha akairejeshea Iran vikwazo katika marhala mbili. Ujerumani, Uingereza na Ufaransa zimeahidi kuyalinda makubaliano hayo ya nyuklia kwa kuidhaminia Iran maslahi yake ya kiuchumi baada ya Marekani kujitoa kinyume cha sheria. 

Trump akitangaza kujitoa katika makubaliano ya JCPOA

Tarehe Nane Mei 2019 serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilichukua uamuzi wa kusimamisha kwa muda utekelezahi wa ahadi zake kuhusiana na makubaliano ya JCPOA ikiwa imepita mwaka mmoja tokea Marekani ijitoe katika makubaliano hayo na kuzipatia nchi za Ulaya muda wa siku 60 kutekeleza ahadi zake kuhusiana na makubaliano hayo ya nyuklia.  

 

Tags