Russia yapinga kuwepo majeshi ya nchi za kigeni Ghuba ya Uajemi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i54962-russia_yapinga_kuwepo_majeshi_ya_nchi_za_kigeni_ghuba_ya_uajemi
Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa kuwepo majeshi ya kigeni katika eneo la Ghuba ya Uajemi kunasababisha hatari ya kutokea vita.
(last modified 2025-10-23T11:19:28+00:00 )
Jul 24, 2019 08:15 UTC
  • Russia yapinga kuwepo majeshi ya nchi za kigeni Ghuba ya Uajemi

Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa kuwepo majeshi ya kigeni katika eneo la Ghuba ya Uajemi kunasababisha hatari ya kutokea vita.

Vasily Nebenzya amekiambia kikao cha Baraza la Usalama mjini New York kwamba, kuongezeka majeshi ya nchi za kigeni katika eneo la Ghuba ya Uajemi kunazidisha hatari ya kutokea vita na kunaweza kuwa na matokeo yenye uharibifu mkubwa. 

Vasily Nebenzya ameongeza kuwa mgogoro katika eneo la Ghuba ya Uajemi unahatarisha amani ya kanda hiyo na juhudi za kimataifa za kukomesha machafuko. 

Mwakilishi wa Rusia katika Umoja wa Mataifa amesema kwa sasa tunashuhudia ongezeko la majeshi ya nchi ambazo si za Ghuba ya Uajemi katika eneo hilo, suala ambalo linazidisha hatari ya kutokea vita vyenye uharibifu mkubwa. 

Katika sehemu nyingine Nebenzya amekosoa uharifu wa nyumba za Wapalestina unaofanywa na Israel na kusisitiza udharura wa kutazamwa vyema suala hilo.