Guterres aitaka Israel ikomeshe ukiukaji wa haki za binadamu huko Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/world-i57265-guterres_aitaka_israel_ikomeshe_ukiukaji_wa_haki_za_binadamu_huko_palestina
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel ukomeshe ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya raia wa Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 14, 2019 06:38 UTC
  • Antonio Guterres
    Antonio Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel ukomeshe ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya raia wa Palestina.

Antonio Guterres ameitaka Israel kufuata kanuni na kutotumia mbinu zinazopingana na sheria za kimataifa dhidi ya Wapalestina.

Matakwa hayo ya Guterres yamewekwa katika ripoti ya kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa iliyotayarishwa kuhusiana na ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa Palestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ikiwemo Quds tukufu.

Katika ripoti hiyo Antonio Guterres ameitaka Israel iheshimu haki za watoto wa Kipalestina na kwamba mienendo ya maafisa wa utawala huo na watoto hao inapaswa kuoana na umri wao.

Vilevile Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala Kizayuni wa Israel ufungue haraka vivuko vinavyoelekea Ukanda wa Gaza na kuahidi kuwapa Wapalestina uhuru wa kutembea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na utawala huo.  

Matakwa hayo ya Antonio Guterres yametolewa baada ya Israel kuanzisha mashambulizi makali dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza tangu Jumanne iliyopita.

Israel imeua makumi ya raia wa Gaza tangu Jumanne iliyopita

Hadi sasa mashambulizi hayo yameua shahidi raia wasiopungua 32 wa Palestina akiwemo kamanda wa tawi la kijeshi la harakati ya Jihad Islami ya Palestina, Baha Abu al-Ata. Raia wengine zaidi ya mia moja wamejeruhiwa.