Venezuela: Vikwazo vya Marekani ni ukiukaji wa sheria za kimataifa
(last modified Thu, 21 Nov 2019 01:05:10 GMT )
Nov 21, 2019 01:05 UTC
  • Venezuela: Vikwazo vya Marekani ni ukiukaji wa sheria za kimataifa

Venezuela imetangaza kuwa mamilioni ya dola ambazo ni mali ya wananchi wa nchi hiyo zimeathiriwa na hatua za vitisho na za upande mmoja za Marekani; na huo ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.

Felix Plasencia Waziri wa Sheria na Biashara ya Nje wa Venezuela ameeleza kuwa Caracas imeshindwa kupata mamilioni ya dola ambazo ni mali ya nchi hiyo zilizoko nje ya nchi kutokana na vikwazo vya upande mmoja vya Marekani dhidi ya nchi hiyo. Kiongozi huyo wa Venezuela ameongeza kuwa: Hatua hiyo ya Washington ni aina fulani ya jitihada za kuitwisha nchi huru na inayojitegemea maamuzi yake ya upande mmoja. Plasencia amesema kuwa, wameathirika kwa kushindwa kurejesha fedha zao hizo. Ameongeza kuwa, fedha za Venezuela kama vile mapato yanayotokana na uuzaji mafuta zimezuiwa huko Marekani. 

Serikali ya Marekani imeiwekea vikwazo mbalimbali Venezuela tangu kuanza mwaka huu wa 2019  ili kumlazimisha Rais wa nchi hiyo Nicolaus Maduro aondoke madarakani. 

Rais Nicolaus Maduro wa Venezuela

Vikwazo vya Marekani vimeilenga pakubwa sekta ya mafuta ya Venezuela; ambayo inaunda sehemu kubwa ya uchumi wa nchi hiyo. 

Tags