Baadhi ya mabalozi na wanadiplomasia wahamishwa kutoka Korea Kaskazini
(last modified Tue, 10 Mar 2020 02:37:00 GMT )
Mar 10, 2020 02:37 UTC
  • Baadhi ya mabalozi na wanadiplomasia wahamishwa kutoka Korea Kaskazini

Sambamba na kushadidi hatua za serikali ya Korea Kaskazini za kukabiliana na virusi vya Corona, ndege maalumu ya nchi hiyo imewaondoa makumi ya wanadiplomasia na raia wa kigeni kutoka nchi hiyo na kuwapeleka katika uwanja wa ndege wa mashariki mwa Russia.

Taarifa iliyotolewa leo na idara ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Vladivostok imesema kuwa, ndege iliyokuwa imebeba makumi ya mabalozi na raia wa nchi za kigeni kutoka Pyongyang, mji mkuu wa Korea Kaskazini ilitua majira ya asubuhi katika uwanja wa ndege wa mji huo.

Tarehe Pili mwezi huu serikali ya Pyongyang iliondoa karantini ya mwezi mmoja kwa ajili ya wanadiplomasia wa kigeni walioko nchini humo ili ikilazimika waweze kuondoka Korea Kaskazini.

Kiongozi wa Korea Kaskazini

Televisheni ya CNN ya Marekani pia imeripoti kwamba kunaendelea kufanywa mpango mwingine wa kuwaondoa wanadiplomasia 60 wa nchi za kigeni utoka nchi hiyo.

Hadi sasa Korea Kaskazini bado haijatangaza rasmi kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona. Hata hivyo vyombo vya habari vya nchi hiyo vimetangaza kuwa maelfu ya watu wamewekwa karantini kwa lengo la kuzuia maambukizi ya virusi hivyo.

Tags