Malengo ya kuhamishwa wanajeshi wa Marekani nchini Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/world-i60095-malengo_ya_kuhamishwa_wanajeshi_wa_marekani_nchini_iraq
Katika siku chache za hivi karibuni kuwekuwepo operesheni kabambe ya kuhamishwa wanajeshi wa Marekani kutoka sehemu moja ya kupelekwa jingine ndani ya ardhi ya Iraq.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 01, 2020 06:44 UTC
  • Malengo ya kuhamishwa wanajeshi wa Marekani nchini Iraq

Katika siku chache za hivi karibuni kuwekuwepo operesheni kabambe ya kuhamishwa wanajeshi wa Marekani kutoka sehemu moja ya kupelekwa jingine ndani ya ardhi ya Iraq.

Swali muhimu linaloulizwa ni kwamba, ni yepi malengo ya kuhamishwa huko kwa wamajeshi wa Marekani ndani ya ardhi ya Iraq ambako kunaambatana na propaganda na makelele mengi ya vyombo vya habari?

Tunaweza kutoa sababu nne kuhusiana na suala hilo. Kwanza ni kwamba, takwimu za kimataifa zinaonyesha kuwa, Marekani ambayo ina wagonjwa zaidi ya 166,846 wa virusi hatari vya corona, inashika nafasi ya kwanza duniani na wagonjwa 3,431 miongoni mwao wamefriki dunia. Uzembe na kufeli kwa serikali ya Donald Trump katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona kumezusha malalamiko na ukosoaji mkubwa ndani ya Marekani. Spika wa Bunge la nchi hiyo, Nancy Pelosi amesema kuwa, hatua ya Donald Trump ya kukanusha uhakika na ukweli wa mambo na kuchelewa kuchukua hatua na maamuzi muhimu ya kukabiliana na janga hilo kumesababisha vifo vya maelfu ya raia wa Marekani. Pelosi ameongeza kuwa, baada ya kumalizika mgogoro wa sasa wa virusi vya corona kuna ulazima kufanyika uchunguzi kuhusiana na jinsi Trump alivyoamiliana na mgogoro huo.

Donald Trump

Kwa kutilia maanani haya yote inaonekana kuwa, serikali ya Donald Trump inatumia mbinu hii ya kuhamisha idadi kubwa ya wanajeshi kutoka eneo moja na kwenda jingine tena kwa propaganada kubwa za vyombo vya habari ili kuzipotosha fikra za waliowengi kuhusiana na kufeli kwa serikali yake katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.  

Pili ni kwamba, katika miezi ya hivi karibuni hususan baada ya jinai ya mauaji ya kigaidi ya Marekani dhidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, kumeshuhudiwa kushadidi vitisho dhidi ya wanajeshi wa Marekani katika ardhi ya Iraq. Inaonekana kuwa, Wamarekani wamechukua uamuzi wa kuondoka katika kambi za kijeshi za al Anbar na al Qayara huko kusini mwa Mosul na vilevile kambi ya K1 katika eneo la Kirkuk ili kupunguza idadi ya kambi zao za jeshi nchini Iraq na baadala yake kuhamia katika kambi ya jeshi ya Ainul Asad na kambi nyingine zenye usalama mkubwa zaidi.

Tatu ni kuwa, Iraq bado haijawa na baraza jipya la mawaziri na kwa sasa serikali ya waziri mkuu aliyejiuzulu, Adil al Mahdi, inaendelea kusimamia masuala ya serikali. Katika hali hii Rais Barham Saleh wa Iraq amemteuwa Adnan al-Zurfi kuwa waziri mkuu mpya na uteuzi huu umepingwa na baadhi ya makundi muhimu ya Iraq hususan makundi yenye mfungamano mkubwa na harakati ya wananchi ya al Hashdul Shaabi ambayo yanamtambua al Zarfi kuwa ni mtu wa Marekani. Upinzani huu umeongezeka sana katika siku za hivi karibuni na hata makundi mbalimbali ya kisiasa ya Iraq yamependekeza mtu mwingine badala ya Adnan al Zarfi.

Mfumo wa makombora wa Patriot wa Marekani

Inaonekana kuwa, operesheni ya kuhamisha majeshi ya Marekani kutoka kambi hii na kulekea kambi nyingine tena kwa makelele mengi ya vyombo vya habari inafanyika kwa shabaha ya kuyatia woga na hofu makundi ya kisiasa ya Iraq na kama vita vya kisaikolojia na kinafsi dhidi ya makundi hayo ili yaache kukwamisha uundaji wa baraza jipya la mawaziri chini ya uongozi wa Adnan al Zarfi.

Nne ni kwamba, kuna uwezekano wa kufanyika mashambulizi makubwa ya kijeshi dhidi ya makundi ya muqawama na yanayopinga sera za Marekani nchini Iraq. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, katika miezi ya hivi karibuni Marekani imepata vipigo mtawalia kutoka kwa makundi hayo ya Iraq, na kipigo cha hivi karibuni zaidi ni mauaji ya wanajeshi wake wawili katika shambulizi lililolenga kambi ya wanajeshi wa nchi hiyo ya al Taji.

Tukiachilia mbali maudhui ya nini malengo ya kuhamishwa majeshi ya Marekani kutoka kambi moja na kwenda nyingine huko Iraq inatupasa kusisitiza kuwa, hatua hiyo peke yake ni ukiukaji mkubwa wa mamlaka ya kujitawala ya Iraq na tishio kwa usalama na amani ya nchi hiyo.