Amnesty International yataka kufanyike uchunguzi kuhusu mlipuko wa Beirut
https://parstoday.ir/sw/news/world-i62650-amnesty_international_yataka_kufanyike_uchunguzi_kuhusu_mlipuko_wa_beirut
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa kuhusu mlipuko mkubwa uliotokea katika bandari ya Beirut nchini Lebanon.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 06, 2020 09:32 UTC
  • Amnesty International yataka kufanyike uchunguzi kuhusu mlipuko wa Beirut

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kimataifa kuhusu mlipuko mkubwa uliotokea katika bandari ya Beirut nchini Lebanon.

Taarifa iliyotolewa leo na shiriki hilo imetaka kuchukuliwe hatua za haraka za kimataifa za kuchunguza mlipuko wa Beirut na kusema: Picha za kutisha za baada ya mlipuko huo zimeonyesha uharifu mkubwa, na Amnesty International inaelekeza macho yake zaidi kwa wahanga wa tukio hilo na familia zao katika kipindi hiki cha majonzi.

Maafisa wa serikali ya Lebanon tayari wameanzisha uchunguzi kuhusu mlipuko huo mkubwa uliotokea juzi jioni katika bandari ya Beirut.

Inaripotiwa kuwa moto uliotokea katika maghala ya mada za milipuko katika bandari hiyo ulisababisha mlipuko mkubwa katika maghala mengine jirani na eneo hilo yaliyokuwa na mada za Ammonium Nitrate.

Mlipuko wa bandari ya Beiruti umesababisha hasara kubwa.

Wizara ya Afya ya Lebanon imetangaza kuwa, hadi sasa mlipuko huo umesababisha vifo vya watu 150 na kujeruhi karibu wengine elfu tano. 

Lebanon imetangaza siku tatu za maombolezo ya taifa na  jeshi la nchi hiyo limepewa jukumu la kudhamini usalama wa Beirut. Aidha imeamuliwa kuwa, sheria ya hali ya hatari iendelee kutekelezwa mjini Beirut kwa muda wa wiki mbili.