Mahakama ya Kimataifa ya Hague: Hizbullah haikuhusika katika mauaji ya Hariri
https://parstoday.ir/sw/news/world-i62892-mahakama_ya_kimataifa_ya_hague_hizbullah_haikuhusika_katika_mauaji_ya_hariri
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) huko ya The Hague nchini Uholanzi imetoa hukumu ikisema kuwa harakati ya Hizbullah ya Lebanon haikuhusika katika mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon, Rafiq al Hariri.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 18, 2020 21:56 UTC
  • Mahakama ya Kimataifa ya Hague: Hizbullah haikuhusika katika mauaji ya Hariri

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) huko ya The Hague nchini Uholanzi imetoa hukumu ikisema kuwa harakati ya Hizbullah ya Lebanon haikuhusika katika mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon, Rafiq al Hariri.

Taarifa iliyotolewa na mahakama ya ICC imesema kuwa, mauaji ya Rafiq al Hariri yalikuwa operesheni ya kigaidi iliyofanyika kwa malengo ya kisiasa. Imesema kuwa, hakuna ushahidi wowote unaothibitisha kwamba viongozi wa Hizbullah na Syria walihusika katika mauaji ya kigaidi ya waziri mkuu huyo wa zamani wa Lebanon.

Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu amesema hakuna ushahidi wa aina yoyote unaoonesha kuwa, harakati ya Hizbullah ya Lebanon ilihusika na mauaji hayo. Amesisitiza kuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah, alikuwa na uhusiano mzuri na Rafiq al Hariri. 

Rafiq Hariri

Waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafiq al Hariri na wenzake 21 waliuawa katika mlipuko wa bomu uliotokea tarehe 14 Februari mwaka 2005 mjini Beirut. Watu wanne walitiwa nguvuni kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo ya kigaidi. 

Baada ya tukio hilo Umoja wa Mataifa ulianzisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo katika mahakama maalumu kwa ajili ya Lebanon.