Grossi: Safari yangu Iran ilikuwa ya mafanikio
https://parstoday.ir/sw/news/world-i63054-grossi_safari_yangu_iran_ilikuwa_ya_mafanikio
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ametangaza kuwa, tarehe iliyoafikiwa kati ya wakala huo na Iran kwa ajili ya IAEA kufanya uhakiki ipo karibu sana.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 27, 2020 01:59 UTC
  • Grossi: Safari yangu Iran ilikuwa ya mafanikio

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ametangaza kuwa, tarehe iliyoafikiwa kati ya wakala huo na Iran kwa ajili ya IAEA kufanya uhakiki ipo karibu sana.

Akijibu suali la waandishi wa habari leo asubuhi kuhusu mapatano yaliyofikiwa baina na wakala huo na Iran kwa ajili ya kuyafikia na kuyakagua maeneo mawili yaliyoainishwa  baada ya kumalizika safari yake ya siku mbili hapa Tehran, Rafael Grossi amesema kuwa na hapa ninamnukuu" sisi kwa kawaida hatuweki wazi tarehe hasa kwa sababu sehemu ya taarifa za mapatano ni ya siri lakini ninaweza kusema kwamba sisi tumekubaliana kuhusu suala hil na muda wa jambo hilo upo karibu sana."  

Rafael Grossi katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje Muhammad Javad Zarif 

Akijibu suali kwamba je anataraji kuwa Iran itaruhusu kufikiwa kikamilifu maeneo hayo tajwa kama inavyopaswa kuwa, Mkurugenzi Mkuu wa IAEA amesisitiza kuwa ana uhakika kamili kuhusu suala hilo na akasema: "Hakuna vizuizi vyovyote vilivyowekwa." 

Taarifa ya pamoja ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) imesisitiza juu ya suala la kuimarisha ushirikiano wa pande mbili na kuaminiana pande hizo ili kuwezesha kutekelezwa kikamilifu mapatano kamili ya usalama na protokali ya ziada; ambayo yanatekelezwa kwa muda na Iran tangu Januari 16, 2016. 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekanusha mara kadhaa madai  kwamba inaendesha miradi ya siri ya nyuklia na kusisitiza kuwa inaendeleza shughuli zake za nyuklia kwa ajili ya matumizi ya amani na chini ya sheria na usimamizi wa wakala wa IAEA.