Serikali ya Biden kuangalia upya vikwazo walivyowekewa maafisa wa ICC
https://parstoday.ir/sw/news/world-i66166-serikali_ya_biden_kuangalia_upya_vikwazo_walivyowekewa_maafisa_wa_icc
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani amesema kuwa serikali ya nchi hiyo imepanga kuangalia upya vikwazo vya Washington dhidi ya maafisa wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 27, 2021 08:38 UTC
  • Serikali ya Biden kuangalia upya vikwazo walivyowekewa maafisa wa ICC

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani amesema kuwa serikali ya nchi hiyo imepanga kuangalia upya vikwazo vya Washington dhidi ya maafisa wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani ameeleza kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya maafisa wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) vimepangwa kuangaliwa upya licha ya nchi hiyo kupinga hatua zilizochukuliwa na mahakama ya ICC kuhusu jinai za kivita zilizofanywa na wanajeshi wa Marekani huko Afghanistan na jinai za kivita za utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Palestina.  

Tarehe 11 mwezi Juni mwaka jana Marekani iliwawekea vikwazo maafisa wa ICC kufuatia uchunguzi uliofanywa kuhusu uwezekano wa wanajeshi wa Marekani kutekeleza jinai za kivita huko Afghanistan. 

Jitihada za Bi Fatou Bensouda Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama hiyo ya Hague Uholanzi kwa ajili ya kuchunguza jinai za kivita za utawala wa Kizayuni katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Ukanda wa Ghaza pia zilikabiliwa na radiamali ya viongozi wa serikali ya zamani ya Marekani. 

Fatou Bensouda, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya ICC