Noam Chomsky: Marekani imepoteza nguvu zake duniani
Noam Chomsky, msomi na mwananadharia mashuhuri nchini Marekani amesema nchi hiyo imepoteza nguvu ilizokuwa nazo duniani.
Kwa mujibu wa toleo la leo la gazeti la The Guardian, Chomsky ameeleza hayo katika makala aliyoandika katika tovuti ya TomDispatch. Katika makala yake hiyo mwanafikra huyo ameuliza suali:"Nani anatawala dunia?", kisha anatoa jibu kwa kusema 'sio tena Marekani'.
Noam Chomsky, ameongeza kuwa Marekani imetingwa na changamoto za kila upande na kupoteza nguvu na satua yake duniani na kwamba mbele ya fikra za walimwengu imegeuka kuwa "dola namba mbili lenye nguvu zaidi duniani".
Katika makala yake hiyo Chomsky amezigawa changamoto zijazo katika makundi matatu ya Mashariki ya Asia, Mashariki ya Ulaya na Ulimwengu wa Kiislamu na kulitolea maelezo na ufafanuzi kila moja kati ya makundi hayo. Makala hiyo ya Noam Chomsky ni sehemu ya kitabu chake kipya kuhusu nguvu za Marekani na hali ya ulimwengu kiitwacho "Nani anatawala dunia?".../