Idadi ya watoto wanaosumbuliwa na njaa yaongezeka kwa 50% Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i68536-idadi_ya_watoto_wanaosumbuliwa_na_njaa_yaongezeka_kwa_50_marekani
Takwimu za karibuni kabisa nchini Marekani zinaonyesha kuwa idadi ya watoto wanaosumbuliwa na njaa nchini humo imeongezeka kwa asilimia 50.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Apr 01, 2021 02:51 UTC
  • Watoto wanasumbuliwa na njaa Marekani
    Watoto wanasumbuliwa na njaa Marekani

Takwimu za karibuni kabisa nchini Marekani zinaonyesha kuwa idadi ya watoto wanaosumbuliwa na njaa nchini humo imeongezeka kwa asilimia 50.

Ripoti iliyotolewa na tovuti ya Child Hunger inasema kuwa, idadi ya watoto wanaosumbuliwa na njaa nchini Marekani imeongezeka kwa silimia 50 tangu ulipoanza mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona. 

Tovuti hiyo imeripoti kuwa, ongezeko la idadi ya watototo wanaosumbuliwa na njaa nchini Marekani ni ishara ya mfumo dhaifu wa kijamii na hitilafu kubwa za kimatabaka nchini humo. 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, hitilafu zinazoshuhudiwa katika Kongresi ya Marekani ndiyo sababu ya kuendelea matatizo makubwa katika kuandaa mahitaji muhimu ya familia mbalimbali katika kipindi hiki cha maambukizi ya corona. 

Watoto wengi wanasumbuliwa na njaa Marekani

Mwaka jana wa 2020 mchambuzi maarufu wa Marekani, Michael Snyder alisema katika ripoti yake kwamba, bei ya bidhaa za chakula zinapanda kwa kiwango cha kutisha nchini Marekani na kwamba kutokana na wimbi la maambukizi ya corona, makampuni makubwa yanashindwa kuzalisha kiwango kinachohitajika cha mahitaji ya watu. 

Marekani inaongoza duniani kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya waathirika na wahanga wa virusi vya corona, na hadi sasa Wamarekani zaidi ya laki tano na 65 elfu wameaga dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19.