Ujerumani yakariri msimamo wake wa kiuhasama dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/world-i75398-ujerumani_yakariri_msimamo_wake_wa_kiuhasama_dhidi_ya_iran
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani kwa mara nyingine tena amekariri msimako wa kiuhasama wa Berlin dhidi ya Tehran na mapatano ya nyuklia ya JCPOA bila ya kuashiria hatua ya Marekani ya kujitoa kwa upande mmoja katika mapatano hayo, na nchi za Ulaya kutotekeleza majukumu yao kwa mujibu wa mapatano hayo ya kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 04, 2021 22:51 UTC
  • Ujerumani yakariri msimamo wake wa kiuhasama dhidi ya Iran

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani kwa mara nyingine tena amekariri msimako wa kiuhasama wa Berlin dhidi ya Tehran na mapatano ya nyuklia ya JCPOA bila ya kuashiria hatua ya Marekani ya kujitoa kwa upande mmoja katika mapatano hayo, na nchi za Ulaya kutotekeleza majukumu yao kwa mujibu wa mapatano hayo ya kimataifa.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani amepinga maombi ya Iran kwa Marekani kwa ajili ya kuachilia fedha zake zilizozuiliwa kama sharti la kuanza tena mazungumzo ya JCPOA huko Vienna. Ujerumani imedhihirisha upinzani wake huo sambamba na siasa za Magharibi dhidi ya Iran.  

Hossein Amirabdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Jumamosi wiki hii aliashiria kadhia ya JCPOA na kueleza kuwa: Rais Joe Biden wa Marekani anapasa kuachilia fedha za Iran zilizozuiwa na nchi hiyo ili kuonyesha azma yake ya kweli.

Hadi sasa tayari zimefanyika duru sita za mazungumzo ya moja kwa moja huko kati ya Iran na nchi wanachama katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA huko Vienna Austria ili kuwezesha Marekani kurejea katika mapatano hayo ya kimataifa. 

Kamisheni ya mapatano ya JCPOA 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza kuwa, kwa kuzingatia kwamba Marekani ndiyo iliyokiuka mapatano ya JCPOA, Washington inapasa kwanza kuiondolea Iran vikwazo na kisha irejee katika mapatano hayo na itekeleza ahadi na majukumu yake ili kuweza kujenga hali ya kuaminiwa. Tehran inasisitiza kuwa haina haraka ya Marekani kurejea katika mapatano ya JCPOA.