Takwimu: Vifo vya uzazi vimeongezeka Marekani kutokana na ubaguzi wa rangi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i80720-takwimu_vifo_vya_uzazi_vimeongezeka_marekani_kutokana_na_ubaguzi_wa_rangi
Vifo vya uzazi vya akina mama nchini Marekani, ambayo ndiyo inavyoongoza kwa sasa duniani, vilifikia kiwango cha juu zaidi katika nusu karne mwaka wa 2020, na uwezekano wa kufariki dunia wanawake weusi wenye asili ya Afrika raia wa Marekani ni mara tatu zaidi ya wanawake wa kizungu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 24, 2022 09:05 UTC
  • Takwimu: Vifo vya uzazi vimeongezeka Marekani kutokana na ubaguzi wa rangi

Vifo vya uzazi vya akina mama nchini Marekani, ambayo ndiyo inavyoongoza kwa sasa duniani, vilifikia kiwango cha juu zaidi katika nusu karne mwaka wa 2020, na uwezekano wa kufariki dunia wanawake weusi wenye asili ya Afrika raia wa Marekani ni mara tatu zaidi ya wanawake wa kizungu.

Hayo yameripotiwa na Taasisi za Kitaifa za Afya za Marekani ikitangaza kuwa kiwango cha vifo vya akina mama weusi Wamarekani ni asilimia 55.3, ambayo ni karibu mara tatu zaidi ya akina mama weupe.

Taarifa ya taasisi hiyo inasema kuwa, kiwango cha vifo vya uzazi vya akina mama weupe wa Marekani ni asilimia 19.1.

Ingawa Marekani hutumia zaidi ya mara mbili ya pesa kwa kila mtu katika sekta ya afya kuliko wastani wa nchi zenye kipato cha juu, lakini ina hali tofauti katika viwango vya vifo vya uzazi ikilinganishwa na nchi mfano wake. 

Japokuwa vifo vya uzazi vimepungua duniani kote katika karne ya ishirini, kiwango cha vifo vya akina mama hao kimeongezeka nchini Marekani tangu maka 2000. 

Ongezeko la vifo vya uzazi nchini Marekani liliripotiwa rasmi mara ya mwisho mwaka 1968.