Hillary Clinton aunga mkono makubaliano ya nyuklia, amkosoa Trump
Mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrats, Hillary Clinton ameunga mkono makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa baina ya madola makubwa ya dunia na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Hillary Clinton ametangaza msimamo huo katika hotuba aliyotoa kuhusiana na usalama wa taifa wa Marekani, ambapo mbali na kutangaza uungaji mkono wake kwa makubaliano ya nyuklia na Iran amesema: "lakini Donald Trump, mgombea wa Republicans ameyakosoa makubaliano haya ya kidiplomasia".
Mbali na kupingana na msimamo huo wa Trump, Clinton amehoji akimlenga Trump:"kama yasingefikiwa makubaliano ya nyuklia, ungetaka kuamiliana vipi na Iran?"
Mgombea huyo wa chama cha Democrat amekosoa pia kile alichoeleza kuwa ni misimamo isiyo ya busara na hatari ya Donald Trump kuhusu Shirika la Kijeshi la NATO, Russia na Korea Kaskazini na kueleza kwamba mgombea huyo wa Republican hana ustahiki wa kubeba jukumu ambalo linalazimu kuwa na utambuzi, uchukuaji hatua thabiti na hisi pana za kuelewa mas-ulia.
Clinton aidha ameongeza kuwa Donald Trump hapasi kuwa na mamlaka ya kuzifikia alama za siri za silaha za nyuklia za nchi hiyo.../