UN: Raia zaidi ya elfu tano wameuliwa katika vita Ukraine
-
vita vya Ukraine
Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, raia zaidi ya elfu 5 wameuliwa huko Ukraine tangu kuanza vita nchini humo.
Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa jana ilitangaza kuwa raia elfu 5 na 24 wameuliwa huko Ukraine tangu kuanza vita nchini humo hata hivyo kunan uwezekano wa kuongezeka idadi ya vifo kutokana na vita vinavyoendelea nchini humo.
Wakati huo huo taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa imeripotikuwa raia wengine elfu 6 na 520 wamejeruhiwa vitani huko Ukraine. Miezi mitano imepita sasa tangu kuanza oparesheni za kijeshi za Russia dhidi ya Ukraine huku nchi hiyo ikiwa imeathirika pakubwa kisiasa,, kijeshi, kiuchumi, kijamii na hata kiutamaduni. Wakati huo huo nchi za Magharibi zinaendelea kutuma silaha na zana za kijeshi huko Ukraine.
Serikali ya Russia mara kadhaa imeeleza kuwa kitendo cha nchi za Magharibi cha kutuma silaha huko Ukraine kitapelekea tu mzozo wa nchi hiyo kudumu kwa muda mrefu huku Russia ikitahadharisha kuwa jeshi la nchi hiyo lina uwezo wa kuzisambaratisha silaha na zana hizo za kijeshi.