Jul 24, 2022 11:07 UTC
  • New York Post: Trump hafai tena kuwa rais wa Marekani

Gazeti la Marekani la New York Times limesema katika ripoti kwamba Donald Trump hana sababu yoyote ya msingi ya kujitetea kuhusu uzembe aliofanya kwa makusudii na hivyo kushindwa kuzuia vurugu zilizofanywa na magenge ya uhalifu katika fujo za Januari 6, 2021.

Kwa  mujibu wa gazeti hilo, ni Donald Trump pekee ndiye angeweza kukomesha vurugu zilizofuatia matukio ya Januari 6, kwa sababu ni yeye pekee ndiye angeweza kusikilizwa na magenge hayo. Hata hivyo, alithibitisha kuwa hastahili kuteuliwa tena kuwa rais wa Marekani.

Kulingana na ripoti hiyo, Trump alifanya uchochezi wa kimya kimya. Alitaka jambo moja tu nalo ni kumshinikiza makamu wake Mike Pence kutothibitisha ushindi wa Joe Biden. Alidhani kwamba vurugu za wafuasi wake sugu zingemlazimisha Pence asalimu amri au kwa uchache acheleweshe kutangazwa matokeo ya kura.

Ingawa wasaidizi, washauri na hata familia ya Trump walimshauri kuyaambia magenge ya wafuasi wake ambao wakati huo walikuwa hawadhibitiki tena, kulegeza msimamo na kurudi nyumbani, lakini badala yake alichochea moto kwa kumlaani Mike Pence kwa kutotengua matokeo ya uchaguzi.

Askari walipokuwa wakijaribu kuzuia Congress isivamiwe na magenge ya Trump

Gazeti hilo la Marekani hata hivyo linasema kuwa sasa ni jukumu la Wizara ya Sheria ya Marekani kuamua iwapo huo ulikuwa ni uhalifu au la. Lakini kama suala la hadhi na heshima, Trump amethibitisha kivitendo kuwa hafai tena kuwa rais wa Marekani.

Shambulio lililofanywa na magenge hayo, lilisababisha kusimamishwa kwa muda kikao kilichokuwa kikiendelea kwa ajili ya kuthibitisha matokeo ya uchaguzi wa rais wa Marekani.

Tags