Waziri: Israel inahusika na wimbi la mauaji linaloshuhudiwa Bangladesh
https://parstoday.ir/sw/news/world-i8668-waziri_israel_inahusika_na_wimbi_la_mauaji_linaloshuhudiwa_bangladesh
Serikali ya Bangladesh imesema yumkini kuna mkono wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika wimbi la mauaji linaloendelea kushuhudiwa nchini humo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 07, 2016 07:41 UTC
  • Waziri: Israel inahusika na wimbi la mauaji linaloshuhudiwa Bangladesh

Serikali ya Bangladesh imesema yumkini kuna mkono wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika wimbi la mauaji linaloendelea kushuhudiwa nchini humo.

Asaduzzaman Khan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Bagladesh amesema kuna ushahidi unaobainisha juu ya kuwepo 'njama za kimataifa' za kuwaangamiza wasomi wa kisekula na viongozi wa dini zenye idadi ndogo ya wafuasi katika nchi hiyo ya bara Asia, ambayo aghalabu ya raia wake ni Waislamu.

Waziri huyo ameashiria mkutano uliofanyika kati ya mwanasiasa wa upinzani wa nchi hiyo na wakala wa Idara ya Kijasusi ya Israel na kusema kuwa hiyo ni ithibati kuwa utawala haramu wa Israel unahusika katika wimbi hilo la mauaji. Polisi ya Bangladesh imesema zaidi ya watu 40 wameuawa tangu Januari mwaka jana 2015, katika wimbi hilo la mauaji ya kutisha. Imearifiwa kuwa, aghalabu ya waliouwa ni wanablogu, wasomi na viongozi wa dini na madhehebu za walio wachache nchini himo kama vile Waislamu wa madhehebu ya Shia, Wahindi na Wakristo.

Kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh lenye kuungwa mkono na kufadhiliwa na utawala wa Kizayuni limekuwa likikiri kuhusika na mauaji hayo.