Russia: Ukraine inawaua kikatili mateka wa kivita
https://parstoday.ir/sw/news/world-i90772-russia_ukraine_inawaua_kikatili_mateka_wa_kivita
Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa wanajeshi wa Ukraine wanafanya mauaji ya kikatili dhidi ya mateka wa kivita wa Russia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 20, 2022 23:03 UTC
  • Russia: Ukraine inawaua kikatili mateka wa kivita

Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa wanajeshi wa Ukraine wanafanya mauaji ya kikatili dhidi ya mateka wa kivita wa Russia.

Wizara ya Ulinzi ya Russia imelaani mauaji hayo ya mateka wa vita yanayofanywa na wanajeshi wa Ukraine na imezitaka jumuiya za kimataifa kulaani vikali ukatili huo na kufanya uchunguzi kamili kuhusiana na jinai hiyo.

Ijumaa ya wiki iliyopita pia Wizara ya Ulinzi ya Russia ilitangaza habari ya kunyongwa mateka 10 wa kivita wa Russia huko Ukraine na kuishutumu Kiev kuwa imefanya uhalifu wa kivita, ambao kwa mujibu wa Moscow, umefumbiwa macho na nchi za Magharibi.

Wizara hiyo imeashiria video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ambayo inaonyesha mateka wa vita wa Kirussia wakinyongwa na wanajeshi wa Ukraine. 

Mateka wa kivita wa Russia wakiteswa na wanajeshi wa Ukraine

Kwa mujibu wa Wizara ya Ulinzi ya Russia, mauaji ya kikatili dhidi ya wanajeshi wa Russia waliotekwa Ukraine sio kesi ya kwanza wala uhalifu wa kivita tu, bali limekuwa jambo la kawaida linalofanywa na wajeshi wa Ukraine kwa uungaji mkono kamili wa  utawala wa Kiev na kufumbiwa macho na waitifaki wake wa Magharibi.