Brazil yaipiku Ujerumani Kombe la Dunia
Timu ya Taifa ya Brazil imeipiku Timu ya Taifa ya Ujerumani katika rekodi za Kombe la Dunia la mpira wa miguu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, timu ya taifa ya Braziil ambayo ndiyo timu yenye fakhari kubwa zaidi katika Kombe la Dunia, iliichapa Uswisi mabao 1-0 katika mechi yake pili ya fainali za kombe hilo zinazoendelea nchini Qatar hivi sasa.
Kwa ushindi huo, Timu ya Taifa ya Brazil imefanikiwa kuingia kwenye hatua ya mtoano na kuipiku pia rekodi ya Ujerumani. Timu za Ureno na Ufaransa nazo zimeshaingia kwenye hatua ya mtoano.
Timu ya Ujerumani ilikuwa inashikilia rekodi ya kushinda mara 16 mfululizo katika hatua ya makundi ya Fainali za Kombe la Dunia. Kwa ushindi wake dhidi ya Uswisi, Timu ya Taifa ya Brazil imefanikiwa kuvunja rekodi hiyo kwa kushinda mara 17 mfululizo katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia.