Mauaji ya kutisha Orlando, Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i9112-mauaji_ya_kutisha_orlando_marekani
Watu wasiopungua 50 wameuawa na wengine 53 kujeruhiwa katika ufyatuaji wa risasi uliotokea katika jimbo la Florida nchini Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 13, 2016 03:24 UTC
  • Mauaji ya kutisha Orlando, Marekani

Watu wasiopungua 50 wameuawa na wengine 53 kujeruhiwa katika ufyatuaji wa risasi uliotokea katika jimbo la Florida nchini Marekani.

Kamanda wa polisi ya Orlando ametangaza kuwa, shambulizi hilo linaorodheshwa katika ugaidi wa ndani na kwamba uchunguzi bado unaendelea.

Ripoti zinasema kuwa, mashambulizi ya jana huko Orlando ni moja kati ya matukio yaliyosababisha mauaji makubwa ya ufyatuaji wa risasi katika jamii ya Marekani. Vyombo vya habari vinasema kuwa, mtu aliyefanya shambulizi hilo ni Mmarekani mwenye asili ya Afghanistan aliyejulikana kwa jina la Omar Mateen. Kutokana na wasifu uliotolewa na vyombo vya habari vya Marekani kuhusu utambulisho wa mtu huyo, kumeanzishwa wimbi kubwa la hujuma na mashambulizi dhidi ya Uislamu na Waislamu katika jamii ya nchi hiyo. Hii ni licha ya kwamba, mafundisho ya dini tukufu ya Uislamu yanakataza mauaji ya wanadamu wasio na hatia yoyote. Hata hivyo inasikitisha kuona kuwa, serikali na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi hususan Marekani havitofautishi baina ya watu wanaofanya ugaidi kwa kutumia jina la Uislamu na mafundisho sahihi ya Qur'ani na Mtume Muhammad (saw) wakati vinapolaani na kuzungumzia ugaidi. Njama hii ya kuyahusisha na Uislamu mashambulizi yote ya kigaidi inafanyika kwa makusudi kwa shabaha ya kuharibu na kuipaka matope sura safi ya dini huyo ya Mwenyezi Mungu na wafuasi wake. Vilevile tinasisitiza kwamba, makundi ya kigaidi ambayo hii leo yanaua watu katika nchi mbalimbali ikiwemo Marekani ni matunda ya siasa za Marekani yenyewe za kuyaunga mkono na kuyasaidia makundi ya kitakfiri na kigaidi. Kwani kama si siasa za uingiliaji kati wa Marekani na kutaka kujitanua katika nchi za Kiislamu za Asia na kaskazini mwa Afrika na vilevile himaya na misaada ya Washington kwa makundi ya kitakfiri na kigaidi basi kusingekuwapo harakati na makundi hayo ya kigaidi. Utawala wa Aal Saud huko Saudi Arabia ambao ndio mfadhili mkuu wa makundi ya kitakfiri na kigaidi katika eneo la Mashariki ya Kati ni muitifaki na mshirika mkubwa zaidi wa Marekani katika eneo hilo.

Wakati huo huo mtu anayefaidika zaidi na tukio la jana huko Orlando ni Donald Tramp, mgombea mtarajiwa wa kiti cha rais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican katika uchaguzi ujao. Awali Tramp alitoa wito wa kupigwa marufuku Waislamu kuingia Marekani. Kwa msingi huo Tramp atafanya jitihada kubwa kuhakikisha kunaenea zaidi anga ya woga na hofu nchini Marekani baada ya tukio la jana huko Orlando kwa ajili ya kujipatia kura zaidi za Wamarekani.

Wakati huo huo Tramp na wenzake watachochea zaidi wimbi la hujuma na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu katika vyombo vya habari.

Hapana shaka kuwa serikali ya Marekani pia inatumia anga ya sasa baada ya tukio la Orlando. Uhuru wa kumiliki na kubeba silaha nchini Marekani umekuwa ukitajwa kuwa sababu ya mauaji ya raia elfu 33 kwa mwaka. Katika kipindi cha utawala wake wa karibu miaka 8 sasa Rais Barack Obama amefanya jitihada za kujaribu kubana kwa njia moja au nyingine uhuru wa kubeba silaha za moto lakini lobi na makundi yenye nguvu na ushawishi mkubwa ya watengenezaji na wauzaji silaha yamezuia yamekwamisha jitihada hizo. Obama alifikia kwiango cha kusema kuwa, kushindwa kuweka sheria za kudhibiti ubebaji silaha nchini Marekani ni miongoni mwa maeneo ambako serikali yake ilishindwa na kufeli katika kipindi cha utawala wake.