Papa Francis: Vita vya Ukraine ni Vita vya Dunia
https://parstoday.ir/sw/news/world-i91858-papa_francis_vita_vya_ukraine_ni_vita_vya_dunia
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani amesisitiza kuwa, vita vya Ukraine ni vita vya dunia na havitakwisha hivi karibuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 18, 2022 23:31 UTC
  • Papa Francis: Vita vya Ukraine ni Vita vya Dunia

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani amesisitiza kuwa, vita vya Ukraine ni vita vya dunia na havitakwisha hivi karibuni.

Papa Francis amesema katika mahojiano na gazeti la ABC la Uhispania kuwa vita vya Ukraine havitamalizika hivi karibuni na kwamba, pande kadhaa zinapigana katika vita hivyo. 

Papa Francis ambaye hivi karibuni alituma ujumbe kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Amani amesisitiza kuwa, vita vya Ukraine ni pigo kwa binadamu na vimeiathiri dunia nzima kwa ujumla.  

Imetimia karibu miezi kumi tangu kuanza vita huko Ukraine vilivyoambatana na taathira kubwa za kisiasa, kijeshi, kiuchumi, kijamii na hata kiutamaduni; huku nchi za Magharibi zikiendelea kutuma silaha na zana za kijeshi nchini humo.  

Russia imeeleza mara kadhaa kwamba, hatua ya nchi za Magharibi ya kutuma silaha huko Ukraine itavifanya vita hivyo viendelee kwa muda mrefu na kuwa na taathira zisizo tabirika.

Jeshi la Russia lilianzisha oparesheni ya kijeshi dhidi ya Ukraine Februari 24 mwaka huu kufuatia ombi la viongozi wa maeneo ya Luhansk na Donetsk ili kukabiliana na mashambulizi ya Ukraine.  

Majimbo ya Luhansk na Donetsk