Feb 18, 2023 07:38 UTC
  • Utafiti: Idadi ya vijana wanaojiua nchini Marekani yaongezeka

Imeelezwa kuwa, idadi ya vijana wanaojiua nchinii Marekani imeongezeka mno katika katika kipindi cha janga la virusi vya Corona.

Utafiti uliofanywa na wahakiki wa kituo cha kuzuia kujiua na utafiti wa hospitali za watoto nchini Marekani unaonyesha kuwa, idadi ya vijana wanaojiua imeongezeka mno nchini humo na kuzua wasiwasi mkubwa katika jamii ya nchi hiyo.

Utafiiti huo unaonyesha kuwa, matukio ya vijana kujiua nchini Marekani yaliongezeka sana wakati wa kushadidi janga la Corona nchini Marekani.

Aidha kwa mujibu wa utafiti huo, mwaka 2020 ciajana 5,568 walijiua katika kipindi cha janga la corona ambapo asilimia 79 kati yao walikuwa vijana wa kiume.

Wakati huo huo, matokeo ya utafiti uliofanya huko Marekani yanaonyesha kuwa mawazo na fikra za kutaka kujiua zimeongezeka sana kati ya watoto na vijana wa nchi hiyo.

Kujitoa uhai, tatizo kubwa miongoni mwa vijana wa Marekani

 

Matokeo ya utafiti huo yaliyochapishwa katika jarida la matibabu la Pediatrics yanaonyesha kuwa idadi ya watu wanaolazimika kufika katika vituo vya matibabu vya Marekani imeongezeka kwa kasi kutokana na tabia ya watoto na vijana kutaka kujiua.

Kwa mujibu wa utafiti huo, idadi ya watoto na vijana waliofika katika vituo hivyo vya matibabu kushughulikiwa tatizo hilo iliongezeka kwa asilimia 59 kutoka mwaka wa masomo wa 2016-2017 hadi 2019-2020.

Ingawa janga la corona linaelezwa kuwa, limeongeza mawazo ya kutaka kujiua miongoni mwa watoto na vijana wa Marekni katika miaka ya hivi karibuni, lakini utafiti unaonyesha kuwa tatizo hilo lilianza kabla ya janga la covid-19.

Tags