May 31, 2023 09:25 UTC
  • Volker Turk
    Volker Turk

Kamishna Mkuu wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya watu wanaotafuta hifadhi nchini Uingereza na Marekani.

Volker Turk, aliyekuwa akizungumza na vyombo ya habari mjini Geneva, amesema kwamba ameeleza rasmi wasiwasi wake kuhusu sheria mpya ya uhamiaji ya Uingereza kwa serikali ya London, akisema kuwa sheria hiyo inawazuia watu kuomba hifadhi nchini humo.

Kamishna Mkuu wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa mwezi uliopita wa Aprili, baraza hilo lilieleza rasmi wasiwasi wake kuhusu sheria mpya ya uhamiaji ya Uingereza, kwa kuzingatia haki za kimataifa za wakimbizi na sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Volker Turk pia ameeleza kuwa sheria mpya za uhamiaji za Marekani zinawatatiza sana watu kuomba hifadhi kwenye mpaka wa nchi hiyo.

Miongoni mwa vipaumbele vya Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak, ni kuzuia wakimbizi wanaotafuta hifadhi kuingia nchini humo kwa boti ndogo kupitia njia ya majini ya English Channel kutoka Ufaransa, na kwa sababu hiyo Bunge la Uingereza mnamo Aprili 2023, lilipasisha Mswada wa Uhamiaji Haramu.

Iwapo utapasishwa na Bunge la Juu ka Uingereza na kuwa sheria, muswada huo utaruhusu kuwekwa kizuizini mara moja na kufukuzwa watu wanaotafuta hifadhi wanaoingia nchini humo kinyume cha sheria kwa njia ya boti au kuwahamisha na kupeleka kwenye nchi zinazoitwa "salama" kama vile Rwanda.

Tags