Pars Today
Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz amemfuta kazi waziri wa fedha na hivyo kuisambaratisha serikali ya muungano wa vyama ya nchi hiyo ya Ulaya Magharibi.
Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimetakiwa zizuie hatua za utawala wa Kizayuni wa Israel ya kutekeleza sheria zilizopitishwa na bunge la utawala huo za kuzuia operesheni za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi wa kipalestina, UNRWA ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Mechi kati ya Paris Saint-Germain na Atletico Madrid katika Ligi ya Soka ya Mabingwa wa Ulaya- UEFA- ilikuwa uwanja wa harakati za kuunga mkono Palestina Jumatano usiku.
Serikali ya Ireland imeafiki kuteuliwa balozi wa Palestina kwa mara ya kwanza katika nchi hiyo ya bara Ulaya.
Rais wa zamani Donald Trump ambaye anaongoza kwa mujibu wa kura zilizohesabiswa dhidi ya Makamu wa Rais Kamala Harris katika kinyang'anyiro cha urais wa 2024 tayari amejitangaza kuwa mshindi huku akitazamia kurejea kwa muhula wa pili katika Ikulu ya White House.
Huku Donald Trump akiwa amejitangaza kuwa mshindi katika uchaguzi wa Marekani, wataalamu wa mambo wanasema hakuna tofauti kwa Afrika kuhusu ni nani anayechukua hatamu za uongozi kati ya mgombea wa Wademokrat au Warepublican.
Sambamba na siku ya uchaguzi wa rais nchini Marekani, waungaji mkono wa Palestina wameandamana mjini New York kupinga sera ya serikali ya Marekani kuhusu Palestina.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kwamba watu wawili wameambukizwa aina mpya ya virusi vya homa ya nyani, "Mpox" nchini Uingereza baada ya kukutana na mgonjwa aliyerejea nchini humo kutoka Afrika. Hayo yanatambuliwa kuwa maambukizi ya kwanza ya ugonjwa huo nje ya Bara Afrika.
Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, anaongoza katika mbio za kuwania kuingia Ikulu ya White House dhidi ya Makamu wa Rais, Kamala Harris, huku wawili hao wakiendelea kukabana koo katika kura za majimbo muhimu ya Marekani.
Kituo cha Kimkakati cha Russia cha Tamaduni kimetazamia kuwa Rais wa Marekani Joe Biden yumkini atazusha mzozo wa kimataifa katika kipindi cha miezi miwili iliyosalia ya utawala wake, iwapo naibu wake, Kamala Harris, atashindwa katika uchaguzi wa rais.