-
Mkuu wa WHO alaani shambulio la Marekani na Israel dhidi ya hospitali nchini Iran
Mar 04, 2026 07:40Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, akizungumzia shambulio la mabomu lililofanywa na Marekani na Israel dhidi ya Hospitali ya Gandhi mjini Tehran, amesisitiza kuwa chini ya Sheria za Kimataifa za Kibinadamu, sekta ya afya haipaswi kulengwa kijeshi
-
Kiongozi wa Wademocrat katika Bunge la Marekani ampinga Trump, asema Iran si tishio
Mar 04, 2026 05:34Kiongozi wa chama cha Democrat katika Bunge la Seneti ya Marekani, Hakeem Jeffries, amekemea kwa ukali serikali ya Donald Trump baada ya shambulizi la kijeshi dhidi ya Iran, akisisitiza kuwa hakuna “tishio tarajiwa” kutoka Iran dhidi ya Marekani.
-
Hujuma ya kijeshi dhidi ya Iran inakiuka Kanuni za Umoja wa Mataifa
Mar 04, 2026 04:18Naibu Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema kuwa hujuma ya kijeshi yaliyotumika na Marekani na Israel dhidi ya Iran inakiuka Kanuni za Umoja wa Mataifa.
-
UN yataka ufanyike uchunguzi wa haraka kuhusu wasichana wadogo 167 waliouliwa na US/Israel
Mar 03, 2026 15:06Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ametaka ufanyike uchunguzi wa haraka kuhusu shambulio lililolenga skuli ya msingi ya wasichana katika mji wa Minab kusini mwa Iran.
-
China yaihutubu Magharibi: Uzimeni moto wa vita usio na tija mliowasha dhidi ya Iran
Mar 03, 2026 12:54Waziri wa Mambo ya Nje wa China amesisitizia ulazima wa faili la nyuklia la Iran kuondolewa kwenye wingu la vita.
-
Nara za “Mauti kwa Marekani” zatanda kwenye anga ya barabara za Rome na Vienna
Mar 03, 2026 12:42Mamia ya wanachama wa asasi zinazopinga vita, wanaharakati wa haki za binadamu na wapinzani wa uchokozi wa kijeshi wa Marekani na utawala wa kizayuni dhidi ya Iran wameandamana katika mitaa na barabara kuu za miji ya Rome, Italia na Vienna, Austria huku wakipiga nara na kaulimbiu za “Mauti kwa Marekani”.
-
Wapinzani wa vita waandamana New York kupinga vita vya Trump dhidi ya Iran
Mar 03, 2026 07:18Mamia ya wanaharakati wanaopinga vita wamefanya maandamano makubwa huko Manhattan mjini New York wakilaani mashambulizi ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Wabunge wa Marekani: Netanyahu amemtwisha Trump mpango wake dhidi ya Iran
Mar 03, 2026 05:46Mtandao wa The Hill umewanukuu wabunge waandamizi wa vyama vyote viwili vikubwa vya Marekani, Democtatic na Republican, wakisema kuwa uamuzi wa Donald Trump wa kuanzisha vita dhidi ya Iran umechukuliwa kutokana na imla ya mpango wa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.
-
Katibu Mkuu wa UN: 'Uhamiaji si mgogoro', ahimiza ushirikiano wa kimataifa
Feb 28, 2026 02:33Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amezitolea wito nchi mbalimbali kupinga simulizi zinazochochewa na hofu kuhusu suala la uhamiaji, akisisitiza kwamba "uhamiaji si mgogoro".
-
Wimbi jipya la upinzani dhidi ya vita nchini Marekani; dalili ya kudhoofika zaidi Trump
Feb 28, 2026 02:11Kadiri matamshi ya kivita yanavyozidi kutoka kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, pamoja na baadhi ya maafisa wa utawala wake, wimbi jipya la upinzani dhidi ya uwezekano wa a vita vya kichochezi vya Marekani dhidi ya Iran limeanza kushika kasi.