Jumamosi, tarehe 22 Machi, 2025
https://parstoday.ir/sw/radio/event-i124198-jumamosi_tarehe_22_machi_2025
Leo ni Jumamosi tarehe 21 mwezi mtukufu wa Ramadhani 1446 Hijria, mwafaka na tarehe 22 Machi 2025.
(last modified 2025-03-22T02:11:27+00:00 )
Mar 22, 2025 02:11 UTC
  • Jumamosi, tarehe 22 Machi, 2025

Leo ni Jumamosi tarehe 21 mwezi mtukufu wa Ramadhani 1446 Hijria, mwafaka na tarehe 22 Machi 2025.

Siku kama ya leo miaka 1406 iliyopita Ali bin Abi Talib (as), wasii wa Mtume Muhammad (saw) na mmoja wa Ahlul Bait wa Mtume, aliuawa shahidi.

Siku mbili kabla ya kifo chake, Imam Ali bin Abi Twalib alipigwa upanga kichwani na mmoja wa Khawarij wakati alipokuwa katika sijda akimwabudu Mwenyezi Mungu msikitini katika Swala ya Alfajiri.

Siku kama ya leo Imam Ali (as) aliaga dunia kutokana na majeraha makubwa aliyopata na hivyo kufikia matarajio yake makubwa ambayo alikuwa akiyatamani daima, yaani kuuliwa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu SW.

Kuuawa shahidi Imam Ali bin Abi Twalib (as) kulikuwa msiba mkubwa na usioweza kufidika kwa Uislamu na Waislamu. 

Imam Ali (as) aliwausia wanawe na Waislamu akisema: "Nawausia kumcha Mungu na kuwa na taratibu nzuri katika mambo yenu. Wajalini yatima na muwafanyie mema majirani zenu, kwani nilimsikia Mtume wa Allah (saw) akiusia kuwafanyia wema jirani hadi nikadhani atawarithisha. Shikamaneni na Qur'ani na msiache watu wengine wawatangulie mbele katika kutekeleza mafundisho yake. Itukuzeni Swala, kwani ndiyo nguzo ya dini yenu.." Sala na salamu za Allah jiwe juu ya Imam Ali bin Abi Twalib na Aali zake watoharifu. 

Tarehe 21 Ramadhani miaka 342 iliyopita alifariki dunia faqihi na mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu Sheikh Abu Jaafar Muhammad bin Hassan maarufu kwa jina la Sheikh Hurr al Aamili huko Jabal Amil nchini Lebanon.

Alitokea kuwa miongoni mwa maulama na watafiti wakubwa wa Kiislamu. Sheikh Hurr al Amili ameandika vitabu vingi vya fiqhi na Hadithi, na miongoni mwavyo ni kile cha Wasaailu Shia ambacho kina nafasi maalumu katika duru za elimu ya fiqhi.

Siku kama ya leo miaka 144 iliyopita lilianzishwa Muungano wa Soka wa Kimataifa kwa shabaha ya kusimamia mashindano ya mpira wa miguu kote duniani.

Kabla ya kuundwa muungano huo, mashindano ya soka yalikuwa yakifanyika katika nchi mbalimbali kwa muundo usiokuwa rasmi.

Muungano huo ulibadilisha muundo wake na kujulikana baadaye kwa jina la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na liliandaa pambano rasmi la kwanza la kimataifa mwaka 1901, kati ya timu za Uingereza na Ujerumani.

Katika siku kama hii ya leo miaka 80 iliyopita, yaani tarehe 22 Machi 1945, iliundwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kutokana na mapendekezo ya Farouk, aliyekuwa mfalme wa wakati huo wa Misri.

Hati ya kuanzisha jumuiya hiyo ilitiwa saini na serikali za Syria, Iraq, Saudi Arabia, Misri na Yemen mjini Cairo.

Lengo la kuanzishwa jumuiya hiyo lilikuwa ni kulinda ardhi na kujitawala kwa nchi wanachama na kuwepo ushirikiano wa karibu wa kisiasa kiuchumi na kiutamaduni kati ya nchi hizo. 

Siku kama ya leo miaka 21 iliyopita aliuawa shahidi Sheikh Ahmad Yassin mwanachuoni na mwasisi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) pamoja na watu wengine 10.

Sheikh Ahmad Yassin aliuawa shahidi baada ya kumaliza swala ya Alfajiri katika msikiti mmoja ulioko eneo la Ukanda wa Gaza, wakati aliposhambuliwa na helikopta za utawala wa Kizayuni wa Israel. Sheikh Ahmad Yasin aliasisi harakati ya Hamas mwaka 1987 akishirikiana na wanamapambano wengine kadhaa wa Kipalestina na miaka miwili baadaye alifungwa jela na utawala ghasibu wa Israel.

Mauaji ya mpigania uhuru huyo ambaye alikuwa kiwete na kipofu wakati wa kuuawa kwake, yalidhihirisha tena ugaidi wa kiserikali wa utawala haramu wa Israel. 

Sheikh Ahmad Yassin