1
Ufufuo na Safari ya Kurejea kwa Allah (1)
Hatima ya mja baada ya kifo, ni miongoni mwa masuala yanayomtia wahka na wasiwasi mkubwa mwanadamu. Je, maisha ya mwanadamu ni hayahaya tuliyonayo hapa duniani yanayoanzia kipindi anapozaliwa hadi anapopatwa na mauti, na hakuna maisha mengine baada ya kufariki dunia? Na je, kuletwa kwetu duniani na kisha kufishwa, kumefanyika kwa malengo maalumu?