Apr 05, 2024 02:16 UTC
  • Ijumaa tarehe 5 Aprili 2024

Leo ni Ijumaa tarehe 25 Ramadhani 1445 Hijria sawa na Aprili 5 mwaka 2024.

Siku kama ya leo miaka 439 iliyoyopita yaani 5 Aprili 1585, yalifanyika mauaji ya halaiki katika mji wa Harlem nchini Uholanzi, ambacho kilikuwa kitovu cha wapigania uhuru nchini humo.

Mauaji hayo yalifanyika kwa amri ya Mfalme wa Uhispania. Jumla ya watu elfu sita wanaaminika kuwa waliuawa kwenye shambulio hilo. Hatimaye Uholanzi ilijipatia uhuru kutoka kwa mkoloni Uhispania hapo mwaka 1609.   

Harlem

Katika siku kama hii ya leo miaka 436 iliiyopita alizaliwa mwanafalsafa wa Uingereza, Thomas Habbes. Alihitimu masomo katika Chuo Kikuu Oxford nchini Uingereza na alifanya utafiti mkubwa kuhusiana na falsafa.

Habbes aliathiriwa sana na fikra za mwanafalsafa Mtaliano Niccolò Machiavelli na alijifunza mengi kutokana na yaliyokuwa yakijiri duniani. Aliamini kuwa mfalme alipaswa kuwa na utawala usio na mipaka na kwamba watu hawapaswi kulalamikia mtawala hata kama malalamiko yao ni sahihi na kwamba walalamikaji walipaswa kukandamizwa.

Mwanafalsafa huyo wa Kiingereza alifariki dunia tarehe 4 Desemba mwaka 1679 akiwa na umri wa miaka 91.

Thomas Habbes

Tarehe 5 Aprili miaka 230 iliyopita, aliuawa Georges Danton mmoja kati ya viongozi wa mapinduzi ya Ufaransa.

Danton licha ya kusomea taaluma ya sheria, alikuwa mhamasishaji mzuri katika kipindi cha mapinduzi ya Ufaransa. Danton alikuwa akiamini kuwa, sanjari na kuzuia machafuko na maafa ya kibinadamu, utawala wa kifalme nchini Ufaransa ulipaswa kutokomezwa. Amma Robes Pierre mmoja kati ya vinara wakubwa wa mapinduzi ya Ufaransa ambaye pia alikuwa mshindani wa Danton alichukua uamuzi wa kumtia mbaroni Danton na hatimaye kumuuwa. 

Georges Danton

Na siku kama ya leo miaka 68 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 5 Aprili 1956, yalimalizika mashambulizi ya kinyama ya majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina katika eneo la Ukanda wa Gaza.

Majeshi hayo, tarehe 4 Aprili, yalianza kufanya mashambulio makubwa na kuwauwa watu 56 na kuwajeruhi wengine 30 wengi wao wakiwa wanawake, watoto na wazee katika kipindi cha siku mbili.

Nchi za Magharibi na jamii ya kimataifa hazikutoa radiamali yoyote kuhusiana na jinai hizo za Wazayuni.   

Gaza

 

Tags