Mar 29, 2017 02:58 UTC
  • Jumatano, 29 Machi, 2017

Leo ni Jumatano tarehe 30 Jamadithani 1438 Hijria, sawa 29 Machi, 2017.

Siku kama ya leo miaka 444 iliyopita, Mfalme Charles IX wa Ufaransa alitoa amri ya kihistoria iliyojulikana kama amri ya uhuru, ambayo ilikuwa na maslahi kwa Wakristo wa madhehebu ya Protestanti. Kwa mujibu wa amri hiyo, Waprotestanti wa Ufaransa ambao walijipatia ushindi kwenye vita vya nne dhidi ya Wakatoliki wa nchi hiyo, walikuwa huru kufanya sherehe, ibada na misa zao nchini humo. Vita vya nne vya kidini kati ya Wakatoliki na Waprotestanti vilianza tarehe 16 Julai mwaka 1572 na vilikuwa maarufu kwa jina la Vita vya La Rochelle.

Mfalme Charles IX

Miaka 245 iliyopita katika siku kama ya leo, alifariki dunia Emmanuel Swedenborg, aliyekuwa mwanafikra mkubwa na msomi wa Sweden. Swedenborg alizaliwa mwaka 1688 na baada ya kubobea kwenye taaluma ya hesabati, aliweza kuwa mhandisi mahiri nchini humo. Swedenborg hakutosheka na elimu hiyo, bali alijipinda zaidi na hatimaye alikuwa gwiji kwenye elimu ya falsafa na irfani. Msingi wa falsafa ya msomi huyo ulikuwa kujitenga na dunia ya kimaada na kughiriki katika ulimwengu wa maana na malakuti.

Emmanuel Swedenborg

Tarehe 29 Machi mwaka 1902 yaani siku kama hii ya leo miaka 115 iliyopita alizaliwa Marcel Aymé mwandishi mashuhuri wa Kifaransa. Awali alisoma taaluma ya uhandishi, lakini alilazimika kuacha masomo yake kutokana na kusumbuliwa na maradhi. Baadaye alianza kujihusisha na uandishi katika gazeti na kuondokea kuwa mwandishi mashuhuri. Baadaye alijishughulisha na uandishi wa magazeti na taratibu akaanza kujihusisha na uandishi wa riwaya ambapo alitokea kuwa mashuhuri katika uwanja huo. Marcel Ayme ameandika vitabu kadhaa na kama "Beautiful Image", na "The Green Mare". Marcel Aymé aliga dunia Oktoba mwaka 1967. 

Marcel Aymé

Na miaka 341 iliyopita katika siku kama ya leo vita baina Poland na Ufalme wa Othmania vilifikia tamati kwa ushindi wa ufalme huo na kutekwa sehemu ya ardhi ya Ukraine iliyokuwa chini ya utawala wa Poland. 

Vita vya mwaka 1673