Sep 22, 2021 08:29 UTC
  • Jumatano tarehe 22 Septemba 2021

Leo ni Jumatano tarehe 15 Safar 1443 Hijria inayosadifiana na tarehe 22 Septemba 2021.

Siku kama ya leo miaka 61 iliyopita inayosadifiana na 22 Septemba 1960, nchi ya Mali ilipata uhuru. Karibu miaka 2,000 nyuma, Mali ilikuwa ikingara kwa utamaduni. Kuanzia karne ya 8 hadi ya 16 Miladia, nchi hiyo ilikuwa ni sehemu ya utawala wa Sudan. Baada ya Morocco kuidhibiti sehemu ya utawala wa Sudan ikiwemo Mali, tawala mbalimbali za kijadi zikafanikiwa kutawala nchini humo. Hatimaye baada ya mapambano ya miaka kadhaa dhidi ya mkoloni Mfaransa, nchi hiyo ikajipatia uhuru katika siku kama ya leo.

Bendera ya Mali

Siku kama ya leo miaka 193 iliyopita, inayosadifiana 22 Septemba 1828, Shaka Zulu kiongozi na muasisi wa utawala wa Kifalme wa Zulu nchini Afrika Kusini aliuawa na ndugu zake. Alikuwa kiongozi wa Wazulu aliyebadilisha ukoo mdogo wa Kinguni kuwa kabila au taifa kubwa lililotawala maeneo mapana ya Afrika Kusini hasa Natal ya leo.

Katika siku kama ya leo miaka 161 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 22 Septemba 1860 vilianza vita vya Peking kati ya vikosi vya Uingereza na Ufaransa dhidi ya China. Katika vita hivyo vikosi vya China vilishindwa kutokana na kutokuwa na zana na silaha za kutosha. Mara baada ya China kushindwa kwenye vita hivyo, ilikubali kutia saini makubaliano ya amani kwa shingo upande, na kuwapatia Uingereza na Ufaransa fursa kubwa ya kujizatiti nchini humo.

Siku kama ya leo miaka 41 iliyopita, inayosadifiana na 31 Shahrivar 1359, utawala wa Iraq uliokuwa ukiongozwa na Dikteta Saddam Hussein ulianzisha mashambulizi makubwa ya angani na nchi kavu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Sambamba na kufanya mashambulizi hayo, majeshi ya Iraq yalipora mali katika miji ya mipakani ya nchi hizo mbili. Kwa mnasaba huo kila mwaka kuanzia siku hii ya tarehe 31 Shahrivar Iran huadhimisha 'Wiki ya Kujilinda Kutakatifu" ili kuwakumbuka na kuwaenzi mashujaa wake waliosimama kidete kukabiliana na uchokozi wa uvamizi wa majeshi ya Saddam Hussein.

Shambulizi la Saddam dhidi ya Iran

 

Tags