-
Khalid Mash'al: Palestina haitaruhusu kutekelezwa njama za kuiyahudisha Masjdul-Aqswa
May 18, 2022 07:47Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) nje ya nchi amesisitiza kuwa, Msikiti wa al-Aqswa ni eneo la kidini na ni la Kiislamu kikamilifu na kwamba, wananchi wa Palestina hawataruhusu kutekelezwa njama chafu za kuliyahudisha eneo hilo takatifu.
-
Israel yampiga marufuku kwa miezi minne Khatibu wa Msikiti wa al Aqsa ; asema sitakaa kimya
May 16, 2022 07:44Utawala wa Kizayuni umempiga marufuku kwa miezi minne Khatibu wa Msikiti wa al Aqsa Sheikh Ikrima Sabri kutokanyaga katika eneo la msikiti huo kutokana na kile ulichokitaja kuwa hatua za Sheikh Sabri za kuuteteta Msikiti Mtukufu wa al Aqsa kibla cha kwanza cha Waislamu.
-
Balozi wa Palestina London aitaka Magharibi kukomesha unafiki
May 05, 2022 02:21Mwakilishi wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina nchini Uingereza ameashiria kimya cha nchi za Magharibi mbele ya vitendo vya kikatili vinavyofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Msikiti wa Al-Aqsa na kueleza kuwa, Palestina itakombolewa kutokana na uungaji mkono mkubwa wa watu huru duniani.
-
HAMAS: Operesheni ya Ari'el ni kuwazindua Wazayuni wasivuke mstari mwekundu
May 04, 2022 11:52Kiongozi mmoja wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Msikiti wa al Aqsa ni mstari mwekundu kwa Wapalestina na kwamba Wazayuni hawapaswi kuuvuuka.
-
OIC: Mji wa Quds na Msikiti wa al Aqsa ni mstari mwekundu kwa Umma wa Kiislamu
Apr 26, 2022 07:44Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imesisitiza kuwa, mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas pamoja na Msikiti wa al Aqsa ni mstari mwekundu kwa Umma wa Kiislamu na amani na utulivu hauwezi kupatikana bila ya kukombolewa maeneo hayo matakatifu kutoka kwenye makucha ya utawala wa Kizayuni.
-
Msikiti wa Al Aqsa, utambulisho wa kihistoria na kidini wa Palestina
Apr 24, 2022 08:26Karibu Wapalestina 150,000 walishiriki katika Sala ya Ijumaa iliyopita iliyosaliwa katika Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
UN yataka kuchunguzwa ukatili wa Wazayuni katika Msikiti wa Al-Aqsa
Apr 23, 2022 13:28Msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka na wa wazi kuhusiana na mashambulio ya kikatili ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya waumini wa Kipalestina waliokuwa wakifanya ibada katika Msikiti wa Al-Aqsa.
-
Mufti wa Oman awakosoa viongozi wa Kiarabu wanaofuturu na Wazayuni huku al Aqsa ikitiwa najisi
Apr 21, 2022 02:49Mufti Mkuu wa Oman, Sheikh Ahmed bin Hamad al-Khalili, amepongeza misimamo ya kishujaa ya wanamapambano wanaoendelea kukabiliana na uvamizi wa mara kwa mara wa Israel katika Msikiti wa Al-Aqsa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
-
Sisitizo la Jumuiya ya Mwamko wa Kiislamu kuhusu ulazima wa kukabiliana na jinai za Israel
Apr 17, 2022 10:38Jumuiya ya Kimataifa ya Mwamko wa Kiislamu imetoa taarifa na kulaani hatua za kichokozi na jinai mpya za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina na kusisitiza kuhusu ulazima wa kukabiliana na jinai za utawala huo. Aidha jumuiya hiyo imepongeza muqawama au mapambano ya watu wa Palestina dhidi ya utawala wa Kizayuni.
-
Wamorocco, Wabahrain, Waturuki waandamana kuitetea Aqsa, Syria, Kuwait zatoa kauli
Apr 17, 2022 08:17Wananchi wa Morocco wamefanya maandamano makubwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Rabat kutangaza uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina, sanjari na kulaani kitendo cha utawala haramu wa Israel cha kuuvamia na kuuvunjia heshima Msikiti wa al-Aqsa.