-
Canada yazuia Wairani kushiriki uchaguzi wa rais wa Iran nchini humo
Jun 26, 2024 08:20Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran amesema Wairani walioko katika nchi za Canada na Saudi Arabia hawatapata fursa ya kushiriki uchaguzi wa rais wa mapema unaotazamiwa kufanyika Ijumaa ijayo.
-
Msisitizo wa Iran wa kuondoka bila masharti Marekani kutoka Syria
Jun 26, 2024 03:28Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, ni jambo la dharura kwa vikosi vya Marekani kuondoka kikamilifu, kwa haraka na bila masharti kutoka Syria na kwamba, hatua hiyo ni muhimu kwa ajili ya amani na utulivu wa nchi hiiyo ya Kiarabu.
-
FAO: Iran kuzalisha zaidi ya tani milioni 20 za nafaka
Jun 25, 2024 04:15Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetangaza kuwa, uzalishaji wa nafaka katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran utazidi tani milioni 20 mwaka huu.
-
Mokhber: ACD inaweza kuwa na mchango muhimu katika kuasisi Asia yenye umoja, nguvu na athirifu zaidi
Jun 24, 2024 08:00Kaimu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe katika Jukwaa la Mazungumzo ya Ushirikiano wa Asia yaani Asia Cooperation Dialogue (ACD) la kundi la D-8 hapa njini Tehran kwamba Asia inaweza kuwa chanzo cha mabadiliko chanya katika michakato ya kimataifa na kichocheo kikubwa cha umoja na mshikamano wa kimataifa.
-
Iran yaalani mashambulizi ya kigaidi katika Jamhuri ya Dagestan, Russia
Jun 24, 2024 07:51Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyojiri katika Jamhuri ya Dagestan na kutoa mkono wa pole kwa taifa la Russia na serikali ya nchi hiyo khususan familia za wahanga wa jinai hiyo.
-
Masuala ya kiutamaduni na wanawake; ajenda kuu ya mdahalo wa wagombea wa uchaguzi wa rais wa Iran
Jun 22, 2024 07:24Mdahalo wa tatu wa kisiasa kwa njia ya televisheni wa wagombea wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umefanyika huku wagombea wakibainisha mipango yao ya sera za serikali kuhusu wanawake na uzalishaji wa kiutamaduni nchini.
-
Radiamali ya Iran kwa hatua ya kihasama ya Canada dhidi ya SEPAH
Jun 21, 2024 07:24Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amelaani vikali hatua ya kihasama na kiuadui ya serikali ya Canada dhidi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH).
-
Kamanda: Iran itatoa jibu mwafaka kwa tishio la aina yoyote
Jun 21, 2024 04:31Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu leo hii ina nguvu zaidi kwenye sekta ya ulinzi kuliko wakati wowote ule, na kwamba tishio lolote dhidi ya taifa hili litapata jibu mwafaka na madhubuti.
-
Iran yamuita balozi wa Italia kulalamikia hatua ya Canada dhidi ya IRGC
Jun 21, 2024 04:19Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imemuita balozi wa Italia mjini Tehran ambaye anawakilisha pia maslahi ya Canada hapa nchini, kulalamikia hatua ya serikali ya Ottawa ya kuliweka Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kwenye orodha ya kile inachokiita "makundi ya kigaidi".
-
Iran: Muqawama lazima uifanye Israel ilipe gharama kubwa kwa uvamizi
Jun 20, 2024 22:47Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema makundi ya muqawama yanapasa kutumia nguvu na uwezo wao wote kuufanya utawala wa Kizayuni wa Israel ulipe gharama kubwa kutokana na uvamizi na mashambulizi yake dhidi ya Ukanda wa Gaza.