Jun 26, 2024 06:58 UTC
  • Msisitizo wa Iran wa kuondoka bila masharti Marekani kutoka Syria

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, ni jambo la dharura kwa vikosi vya Marekani kuondoka kikamilifu, kwa haraka na bila masharti kutoka Syria na kwamba, hatua hiyo ni muhimu kwa ajili ya amani na utulivu wa nchi hiiyo ya Kiarabu.

Kwa mujibu wa Shirika la IRNA; Amir Saeed Iravani", Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kikao cha Baraza la Usalama siku ya Jumanne kuhusu hali ya eneo la Magharibi mwa Asia (Mashariki ya Kati) na Syria, sambamba na kuashiria ukaliaji mabavu, vikwazo visivyo vya kibinadamu, kulifanya kuwa la kisiasa suala la kurejea wakimbizii na kuzuia himaya ya kimataifa ya kukarabatiwa Syria alisema, baadhi ya madola ya Magharibi kama Marekani yanahusika katika kuchukua muda mrefu mapigano huko nchini Syria kwa sababu yanataka kutwisha irada yao kwa wananchi wa taifa hilo.

Mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa: Hatujahusika katika hatua yoyote dhidi ya majeshi ya Marekani nchini Syria au kwingineko

Iravani sanjari na kusisitizia mamlaka ya kujitawala, uhuru wa kisiasa, umoja wa ardhi ya Syria kwamba, vinapaswa kuheshimiwa kikamilifu kama maamuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ameeleza kwamba, jamii ya kimataifa haipaswi kuwaacha peke yao wananchi wa Syria katika vita dhidi ya ugaidi, uvamizi wa kigeni na ugaidi wa kiuchumi unaosababishwa na vikwazo visivyo halali.

Vile vile, balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa akizungumzia ulazima wa kuondolewa majeshi yote ya kigeni kutoka Syria amesisitiza kuwa; Iran inalaani vikali uvamizi unaoendelea wa utawala ghasibu wa Israel dhidi ya mamlaka ya kujitawala ya Syria, kuwalenga raia na miundombinu muhimu, na inafungamana na suala la kutatuliwa mgogoro wa Syria kwa njia za kisiasa.

Tags