-
IRIB yashinda tuzo maalumu ya Uhandisi wa Utangazaji ya ABU 2024
Oct 23, 2024 22:48Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB limeshinda tuzo maalumu ya "Uhandisi wa Utangazaji" ya Umoja wa Redio na Televisheni za nchi za Asia na Pasifiki (ABU) ya mwaka 2024.
-
Iran, Ethiopia zajadili BRICS, uhusiano wao na masuala ya kieneo
Oct 23, 2024 06:54Katika mkutano muhimu wa kidiplomasia, Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian amekutana na Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa Ethiopia, ambapo wamejadili masuala muhimu ya pande mbili na kikanda.
-
Iran yaliandikia barua Baraza la Usalama ikilaani chokochoko za US
Oct 22, 2024 03:46Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amekosoa vikali matamshi ya hivi karibuni ya Rais Joe Biden wa Marekani kuhusiana na njama ovu ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Tehran na kusisitiza kuwa, matamshi hayo "yanatia wasiwasi sana na ni ya kichochezi."
-
IRGC: Vikosi vya Ulinzi vya Iran viko tayari kujibu tishio lolote dhidi ya Iran
Oct 21, 2024 08:09Naibu Kamanda wa Uratibu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesisitiza kuwa vikosi vya ulinzi vya nchi hii vimejiandaa kikamilifu kujibu tishio lolote dhidi ya nchi hii kufuatia kupamba moto mivutano katika eneo.
-
Rais wa Iran akosoa unafiki na undumakuwili wa Wamagharibi
Oct 20, 2024 23:25Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian amekosoa vikali undumakuwili wa utawala haramu wa Israel na Marekani akisisitiza kuwa, Wamagharibi wakiongozwa na Tel Aviv na Washington wanaongoza kwa unafiki licha ya madai yao ya kupigania demokrasia, haki za binadamu na uhuru.
-
Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran yalaani kuuliwa kigaidi na Israel mwanamama Muirani huko Beirut
Oct 20, 2024 23:21Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani vikali kitendo cha Israel cha kumuuwa kikatili mwanamke wa Kiirani na mumewe raia wa Lebanon huko Beirut.
-
Onyo la Iran kwa Marekani kuhusu chokochoko tarajiwa ya Israel
Oct 20, 2024 22:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Marekani inapasa kubebeshwa dhima ya shambulio lolote tarajiwa la Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Reuters: BRICS kujadili mpango mpya wa kimataifa wa mabadilishano ya fedha
Oct 20, 2024 03:11Russia itawasilisha pendekezo lake la mfumo mpya wa fedha wa kimataifa kwa mataifa mengine wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya BRICS katika mkutano wa kilele wa kundi hilo utakaofanyika wiki ijayo nchini humo.
-
UN: Uhuru wa maoni na kujieleza umekandamizwa vikali katika vita vya Israel dhidi ya Ghaza
Oct 19, 2024 23:14Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa wa kuchunguza haki ya uhuru wa kutoa maoni na kujieleza amesema, uhuru wa maoni na kujieleza umehatarishwa vibaya zaidi huko Ghaza kuliko ilivyotokea katika mzozo wowote ule wa hivi karibuni, huku waandishi wa habari wakilengwa katika eneo hilo lenye vita na waungaji mkono wa Palestina wakikandamizwa katika nchi nyingi duniani.
-
Mazoezi ya pamoja ya majeshi ya majini ya nchi za Bahari ya Hindi yaanza Iran
Oct 19, 2024 08:13Mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya Majeshi ya Majini ya nchi za Kandokando ya Bahari ya Hindi (IONS) ), "IMEX 2024," yameanza katika eneo la maji ya Iran katika Ghuba ya Uajemi kwa kuvishirikisha vitengo mbalimbali kutoka nchi kadhaa wanachama na waangalizi.