-
Rouhani: Iran itaendelea kupambana na ugaidi
Jul 11, 2016 12:30Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Iran itaendelea kutetea heshima na hadhi ya Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad (saw) kupitia njia ya kupambana na ugaidi bega kwa bega na wananchi na serikali ya Iraq.
-
Iran yawataka Wairaqi waungane ili waweze kuangamiza magaidi wa ISIS
Jul 10, 2016 08:39Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa wito wa kuwepo umoja imara baina ya makundi mbali mbali ya Iraq ili taifa hilo lifanikiwe kuangamiza magaidi wakufurishaji nchini humo na kote katika eneo.
-
Waziri Mkuu wa Iraq awafuta kazi maafisa usalama Baghdad baada ya kuuawa watu 300
Jul 08, 2016 22:56Waziri Mkuu wa Iraq Haider al-Abadi amewafuta kazi maafisa wa ngazi za juu wanaosimamia usalama katika mji mkuu Baghdad kufuatia hujuma ya kigaidi.
-
Hammond akiri, Uingereza ilihusika kuimarisha Daesh
Jul 08, 2016 03:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza amekiri kwamba nchi yake ilifanya makosa wakati wa vita vya Iraq na kwamba suala hilo limechangia katika kuliimarisha na kulipa nguvu zaidi kundi la kigaidi la Daesh.
-
Magaidi washambulia kaburi la mjukuu wa Mtume, waua watu 35 na kujeruhi 60
Jul 08, 2016 00:18Magaidi wa kundi la kitakfiri la Daesh wameshambulia ziara la mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) katika mji wa Balad ulioko umbali wa kilomita 80 kutoka Baghdad na kuua watu wasiopungua 35.
-
Waingereza wataka Blair apelekewe ICC kwa kuivamia Iraq
Jul 07, 2016 10:00Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, asasi za kiraia na familia za wanajeshi wa Uingereza waliouawa nchini Iraq wamefanya maandamano katika mji mkuu London kulaani hatua ya Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Tony Blair ya kuidhinisha uvamizi dhidi ya Iraq mwaka 2003 bila ya kuwepo sababu ya msingi.
-
Iraq yazitahadharisha nchi zinazowafadhili magaidi
Jul 04, 2016 22:59Waziri Mkuu wa Iraq ametoa radiamali yake kwa mashambulizi ya kigaidi yaliyoutikisa mji mkuu wa nchi hiyo Baghdad hivi karibuni na kusisitiza kuwa Baghad itakabiliana vilivyo na vyanzo na wale wote wanaowaunga mkono na kuwasaidia magaidi, licha ya kuwepo matatizo na vizingizi katika mapambano dhidi ya ugaidi.
-
80 wauawa katika mashambulizi ya mabomu Baghdad, Iraq
Jul 03, 2016 02:52Watu wasiopungua 80 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika mashambulizi pacha ya mabomu katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad.
-
UNICEF: Vita vimesababisha maafa kwa watoto wa Iraq
Jun 30, 2016 10:19Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetahadharisha kuwa watoto milioni tatu na laki sita wa Iraq wanakabiliwa na hatari kubwa ya kifo, kujeruhiwa, ukatili wa kingono, kutekwa nyara na kutumikishwa kama wapiganaji kwenye makundi yanayobeba silaha.
-
46 waua na kujeruhiwa katika hujuma dhidi ya msikiti Iraq
Jun 28, 2016 01:58Makumi ya watu wameuawa na kujeruhiwa katika hujuma ya kigaidi dhidi ya msikiti mmoja viungani mwa Baghdad, mji mkuu wa Iraq.