Jun 30, 2016 14:49 UTC
  • UNICEF: Vita vimesababisha maafa kwa watoto wa Iraq

Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetahadharisha kuwa watoto milioni tatu na laki sita wa Iraq wanakabiliwa na hatari kubwa ya kifo, kujeruhiwa, ukatili wa kingono, kutekwa nyara na kutumikishwa kama wapiganaji kwenye makundi yanayobeba silaha.

Katika ripoti yake iliyotolewa leo, UNICEF imeyataka makundi yote nchini Iraq kulinda haki za watoto na kutangaza kuwa, idadi ya ya watoto wa Iraq wanaokabiliwa na hatari ya kubwa ya kifo au kutumiwa vibaya katika vita vya ndani imeongezeka na kufikia milioni 3 na laki sita katika kipindi cha miezi 18 iliyopita.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, mashambulizi ya kundi la kigaidi la Daesh katika maeneo mengi ya kaskazini na magharibi mwa Iraq na operesheni za jeshi la Iraq za kukomboa maeneo hayo vimekuwa na taathira mbaya na maafa. UNICEF imesema kuwa karibu watoto milioni 4 na laki 7 wa Iraq wanahitaji misaada ya kibinadamu.

Maelfu ya watu wameuawa na mamilioni ya wengine kulazimika kuwa wakimbizi nchini Iraq kutokana na hujuma na ukatili wa kundi la kigaidi la Daesh linalofadhiliwa na Saudi Arabia na washirika wake kama Marekani.

Tags