-
Umoja wa Mataifa: Tuna wasiwasi na hali ya wakimbizi DRC
Dec 15, 2018 23:15Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limeelezea wasiwasi mkubwa lilionao kuhusiana na hali mbaya wanayokabiliwa nayo wakimbizi zaidi ya milioni moja katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
UN yalaani kukandamizwa wapinzani Kongo DR kuelekea uchaguzi mkuu
Dec 14, 2018 12:34Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali ukandamizaji, mbinyo na unyanyasaji unaofanywa na maafisa usalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo dhidi ya wapinzani, siku chache kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu.
-
Uchaguzi mkuu wa Kongo DR katika njia panda, hifadhi ya suhula za kupigia kura yateketea
Dec 13, 2018 10:29Uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao umepangwa kufanyika katika siku kumi zijazo upo katika njia panda baada ya moto mkubwa kuteketeza ghala la kuhifadhia vifaa vya kupigia kura.
-
Polisi ya Kongo yafyatua risasi hai kutawanya wafuasi wa mgombea wa upinzani
Dec 13, 2018 04:47Polisi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo jana kwa siku ya pili mfululizo walitumia gesi ya kutoa machozi na kuwafyatulia risasi hai wafuasi wa Martin Fayulu mgombea wa upande wa upinzani ili kuwatawanya na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
-
Magaidi wa ADF waendeleza mauaji Kongo DR kuelekea uchaguzi
Dec 12, 2018 03:05Watu 10 wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na kundi la wanamgambo wa ADF mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Jeshi la Rwanda laua wapiganaji wanne wa kundi la FDRL
Dec 11, 2018 04:42Jeshi la Rwanda limesema askari wake wamekabiliana vikali na wapiganaji wa kundi la waasi wa FDLR waliojipenyeza nchini humo wakitokea katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Mshindi wa Tuzo ya Nobel: Uchaguzi wa Rais Congo yumkini ukasababisha vita vya ndani
Dec 10, 2018 23:08Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel amesema kuwa, uchaguzi wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia wa Congo uliopangwa kufanyika mwezi huu yumkini ukasababisha machafuko na vita iwapo hautakuwa huru, wa haki na wenye amani.
-
Raia 17 wauawa katika mashambulizi ya ADF Kongo DR
Dec 07, 2018 11:09Raia wasiopungua 17 wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na kundi la wanamgambo wa ADF mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Madaktari wajiunga na mgomo nchini Zimbabwe kutaka hali bora
Dec 03, 2018 23:59Sekta kuu ya madaktari wa hospitali za uma wamejiunga na mgomo nchini Zimbabwe wakati nchi hiyo hivi sasa ikijipapatua kutoka katika mgogoro wa kiuchumi.
-
Jeshi la Kongo DR lakabiliana na waasi; lauwa 18 mashariki mwa nchi
Dec 03, 2018 12:05Mapigano kati ya jeshi na waasi watiifu kwa Jenerali muasi wa zamani huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 18. Hayo yameelezwa leo na duru za jeshi la Kongo.