-
Mahakama Kenya yailaumu polisi kwa kifo cha mwandishi habari wa Pakistan
Jul 09, 2024 07:42Mahakama nchini Kenya jana ilitoa uamuzi ikisema kuwa kitendo cha polisi wa nchi hiyo cha kumpiga risasi mwandishi wa habari wa Pakistan mjini Nairobi mwaka 2022 kilikuwa kinyume cha sheria na kinyume na katiba.
-
Ruto achukua hatua za kubana matumizi kufuatia maandamano ya vijana
Jul 06, 2024 02:39Katika hatua za kubana matumizi, Rais William Ruto wa Kenya ametangaza kwamba atapunguza idadi ya washauri wa serikali kwa asilimia 50, huku watumishi wa umma waliofikisha umri wa kustaafu (miaka 60) wakitakiwa kuondoka kazini mara moja.
-
Rais Ruto aagiza kutazamwa upya nyongeza ya mishahara ya serikali
Jul 04, 2024 06:37Mapendekezo ya nyongeza ya mishahara kwa maafisa wa Serikali na wawakilishi wa Bunge la Kenya hayatatekelezwa baada ya Rais William Ruto wa nchi hiyo kuagiza kuangaliwa upya kwa mipango hiyo kufuatia malalamiko ya umma.
-
Maandamano ya vijana Kenya yaendelea, waandamanaji wamtaka Rais Ruto aondoke madarakani
Jul 02, 2024 14:53Vijana wa Kenya, wengi wao wakiwa Generation Z, wamerejea barabarani katika maandamano yaliyopewa jina la #OccupyEverywhere dhidi ya utawala wa Rais William Ruto.
-
UN: Tumeshtushwa na mauaji dhidi ya waandamanaji Kenya
Jun 28, 2024 03:20Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kusikitishwa kwake na maandamano ya ghasia ya kupinga Muswada wa Fedha wa 2024 nchini Kenya, yaliyopelekea makumi ya watu kuuawa.
-
Waandamanaji Kenya wamtaka Rais Ruto ajiuzulu licha ya kuurejesha muswada wa fedha bungeni
Jun 27, 2024 12:42Waandamanaji Kenya wanamtaka Rais wa nchi hiyo William Ruto ajiuzulu licha ya uamuzi wake wa kuuondoa muswada tata wa fedha wa 2024 uliokuwa umedhamiria kuongeza ushuru ili kusaidia kupunguza mzigo wa madeni nchini humo.
-
Maandamano ya vijana yamlazimisha Ruto kuweka kando Muswada wa Fedha 2024
Jun 26, 2024 15:05Rais William Ruto wa Kenya amesema kwamba hatatia saini Muswada wa Fedha 2024 kuwa sheria. Ni baada ya maandamano makubwa ya siku kadhaa yaliyofuatiwa na mauaji ya waandamanaji mjini Nairobi jumanne ya jana.
-
Watu 10 wameuawa Nairobi wakati polisi ilipowafyatulia risasi waandamanaji waliovamia bunge
Jun 26, 2024 02:51Watu 10 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa jana Jumanne wakati polisi walipowafyatulia risasi mamia ya waandamanaji waliovamia majengo ya bunge jijini Nairobi, mji mkuu wa Kenya, kupinga sheria ya iliyopitishwa na wabunge ya kuongeza ushuru.
-
Mamia ya askari polisi wa Kenya watumwa Haiti licha ya ukosoaji
Jun 25, 2024 10:42Askari polisi 400 wa Kenya wameelekea nchini Haiti leo Jumanne kwa ajili ya kwenda kulinda usalama na kurejesha uthabiti katika nchi hiyo ya Caribbean.
-
Kenya yaruhusu kufanyika maandamano kwa masharti
Jun 25, 2024 07:44Kithure Kindiki Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya amewataka vijana wanaoandamana kupinga Muswada wa Fedha wa 2024 kuimarisha amani na usalama, kutobeba aina yoyote ya silaha kutakiwa kuondoka katika maeneo ya mikusanyiko ifikapo saa kumi na mbili jioni.