-
Mudavadi: Kuweka kando Muswada wa Fedha ni sawa na kuangusha Serikali ya Kenya
Jun 22, 2024 06:49Kinara wa Mawaziri wa Kenya, Musalia Mudavadi, amesema Muswada wa Fedha 2024 lazima upitishwe na kutiwa saini na Rais William Ruto kuwa sheria, akisema kinyume na hivyo itakuwa ni sawa na kuangusha Serikali.
-
Polisi wa Kenya washutumiwa kwa kumuua mmoja wa waandamanaji Nairobi
Jun 21, 2024 07:57Asasi za kiraia na mashirika ya kutetea haki za binadamu yameijia juu polisi ya Kenya kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi mmoja wa waandamanaji wanaopinga mpango wa kuongeza ushuru, kodi na tozo.
-
Marekani kuipa Kenya hadhi ya mshirika wake mkuu asiye mwanachama wa NATO
May 23, 2024 07:20Rais Joe Biden wa Marekani anatarajiwa kuipa Kenya hadhi ya mshirika wake mkuu asiye mwanachama wa NATO wakati wa ziara ya kiserikali ya siku tatu ya Rais wa Kenya William Ruto nchini humo, ambaye amekaribishwa na Biden katika Ikulu ya White House mapema leo kabla ya mapokezi rasmi yatakayoanza kwa ukaguzi wa gwaride la heshima na kufikia kielele chake kwa dhifa ya kifahari ya chakula cha usiku.
-
Polisi 200 wa Kenya kupelekwa Haiti Alkhamisi ijayo
May 18, 2024 04:00Polisi 200 wa Kenya watapelekwa nchini Haiti kulinda usalama siku ya Alkhamisi ijayo. Ni baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu mahakamani, ambapo Januarii mwaka huu Mahakama ya juu nchini Kenya ilitangazwa kuwa, mpango wa serikali wa kutuma polisi nchini Haiti kuongoza kikosi cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa ni kinyume na katiba.
-
Kenya na Uganda zaafikiana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta
May 17, 2024 07:24Kenya na Uganda zimekubaliana kujenga kwa pamoja bomba la kusafirishia mafuta kutoka mjini Eldoret katika eneo la Bonde la Ufa nchini Kenya hadi Uganda.
-
Ripoti yafichua: Chama tawala Kenya kiliazimia kuua Azimio la Umoja-One Kenya
May 10, 2024 09:54Vyombo vya habari vya Kenya vimefichua kuwa, mabadiliko ya siri yaliyotayarishiwa miswada ya kufanikisha utekelezaji wa ripoti ya Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (NADCO) iliyowasilishwa majuzi katika Seneti ya nchi hiyo yamefuchua njama ya kuvunja chama cha Azimio la Umoja-One Kenya kinachoongozwa na Raila Odinga.
-
Kenya yatangaza mapumziko nchi nzima Ijumaa ili kuwaomboleza wahanga wa mafuriko
May 09, 2024 07:17Rais William Ruto wa Kenya ametangaza kesho Ijumaa kuwa ni siku ya mapumziko ili kuwaomboleza watu 238 waliopoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyoiathiri nchi hiyo.
-
Mafuriko Kenya yauwa watu 228
May 06, 2024 03:09Idadi ya walioaga dunia kutokana na mafuriko yaliyokumba Kenya imeongezeka hadi 228 huku mamlaka husika zikiendelea kukabiliana na tishio la kimbunga Hidaya.
-
Mkuu wa Majeshi na makamanda tisa waandamizi wa Kenya wafariki katika ajali ya helikopta
Apr 19, 2024 04:43Kenya inaomboleza kifo cha Mkuu wa Majeshi (KDF), Jenerali Francis Omondi Ogolla ambaye ameaga dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea jana Alkhamisi katika eneo la Sindar kwenye mpaka wa Kaunti ya Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet.
-
Utafiti wafichua: Wanawake Kenya wanageuzwa tasa mahospitalini bila idhini yao
Apr 09, 2024 11:12Ripoti mpya iliyotolewa nchini Kenya imebaini kuwa wanawake wanaotafuta huduma za matibabu ya uzazi nchini humo wanafanyiwa ukaguzi wa sehemu za siri, kukatizwa uwezo wa kupata mimba na kufanyiwa upasuaji usiohitajika wanapojifungua, bila idhini yao.