-
Al-Shabaab ya Somalia yaua 5 kwa tuhuma za ujasusi
Oct 10, 2018 11:19Kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab la Somalia lenye mfungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda limewaua kwa kuwamiminia risasi watu watano kwa tuhuma za kufanya ujasusi kwa niaba ya vyombo vya kiintelejensia vya Marekani, Uingereza na Somalia.
-
Aliyekuwa kamanda wa al-Shabaab anyimwa idhini ya kuwania urais Somalia
Oct 06, 2018 00:20Serikali ya Mogadishu imemnyima kibali cha kugombea urais wa jimbo moja la Somalia, aliyekuwa Naibu Kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab na pia msemaji wa zamani wa genge hilo la ukufurishaji, Mukhtar Robow Abu Mansur, ambaye mwaka jana alijisalimisha kwa jeshi la nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
Al Shabab washambulia msafara wa Umoja wa Ulaya, watu 3 wauawa Mogadishu
Oct 01, 2018 11:07Watu watatu wameuawa katika shambulizi la kujilipua kwa bomu lililofanywa na wanachama wa kundi la kigaidi la al Shabab dhidi ya msafara wa Umoja wa Ulaya mjini Mogadishu.
-
Somalia yaitaka UN iiondolee vikwazo vya silaha
Sep 30, 2018 10:35Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Somalia ameutaka Umoja wa Mataifa kuondoa vikwazo vya muda mrefu vya silaha dhidi ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
-
UN yataka nchi za dunia ziwasaidie Wasomali walioathirika na migogoro na ukame
Sep 04, 2018 23:12Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ameitaka jamii ya kimataifa kuendelea kutoa misaada kwa watu walioathirika na migogoro, ukame wa mwaka 2017 pamoja na mafuriko na kimbunga nchini Somalia hivi karibuni.
-
Sita wauawa katika hujuma ya kigaidi Mogadishu, Somalia
Sep 02, 2018 08:53Watu wasiopungua sita wameuawa baada ya gaidi mmoja kushambulia kwa bomu ofisi ya serikali za mitaa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
-
Idadi ya Wasomali waliofukuzwa makwao yaongezeka maradufu
Aug 28, 2018 08:23Idadi ya Wasomali waliolazimika kukimbia makazi yao imeongezeka mwaka huu na maelfu miongoni mwao wamekuwa wakimbizi tena kutoka kwenye makazi yao ya muda walikokimbilia kutokana na vita, ukame na mafuriko.
-
Rais wa Somalia auzulu na kuteua maafisa wapya wa nyadhifa mbalimbali
Aug 17, 2018 11:01Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wa Somalia amefanya mabadiliko mapya kwa kumteua mkuu mpya wa majeshi pamoja na mkuu wa idara ya upelelezi ya nchi hiyo.
-
Wanajeshi 3 Wasomali wauawa katika hujuma ya kigaidi nje ya Mogadishu
Aug 05, 2018 11:03Wanajeshi wasiopungua watatu wa Somalia wameuawa kufuatia hujuma ya kigaidi katika wilaya ya Afgoye iliyo kilomita 30 kaskaini magharibi mwa mji mkuu, Mogadishu.
-
Askari usalama wavamia jengo la wizara ya mambo ya nje ya Somalia
Aug 04, 2018 22:03Duru za habari Somalia zimeripoti kuwa askari usalama wamevamia jengo la Wizara ya Mambo ya Nje katika mji mkuu Mogadishu kwa lengo la kumtia nguvuni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo.